Kuku wangu wa kienyeji wanataga vizuri na kulalia mayai, lakini utotoaji ni hafifu

no nm

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2014
Posts
212
Reaction score
32
Msaada tafadhali,

Kutatua tatizo hilo. Chakula chenye virutubisho vyote wanapata na maji vyakutosha, pia wana sehemu nzuri za kutagia na kutotolea. Kwa ujumla huduma zote wanapata., ila tatizo ni rate ndogo ya kuzaliana.

Nawasilisha
 
Ratio ya jogoo kwa mitetea ni ngapi?
Majogoo wakiwa wachache ni tatizo maana wana overdoziwa

Wakiwa wengi pia ni shida kwani wanaishia kugombana badala ya kupanda.

Hakikisha ratio ni mitetea 10 kwa jogoo mmoja au ikizidi sana iwe 8 kwa 1
 
si kuku wote wana uwezo mzuri wa kuatamia,wachambue wenye uwezo wa kuatamia ndio wawe wanaatamia ila wasio na uwezo wakifikia muda wa kuatamia wanyang'anye mayai
 
Ahsante,Ratio ni kama 1:12 hivi
 
si kuku wote wana uwezo mzuri wa kuatamia,wachambue wenye uwezo wa kuatamia ndio wawe wanaatamia ila wasio na uwezo wakifikia muda wa kuatamia wanyang'anye mayai

Hayo ninayoyaondoa nawapa kuku wengine wazuri ama?
 
unapotaka kuyaondoa hakikisha mikono yako ni mikavu ni vema ukipaka vumbi au majivu au hata ukijifuta na kitambaa kikavu. Na utakapomwekea kuku mwingine atatotoa kama kawaida.
 
Back
Top Bottom