Kuku wangu wamedumaa, msaada wakuu

muzungu

Member
Joined
Aug 8, 2011
Posts
25
Reaction score
2
Poleni na majukumu wakuu,

Nafuga Kuku wa nyama, lakini hadi kufikia Leo wana wiki ya nne maendeleo yao sio mazuri, kwa kifupi wamedumaa! Nilikuwa nawapatia chakula cha CPF lakini hawakui kama mashamba mengine yanavyokuwa. Pia natumia vitastress kama vitamin.

Msaada wakuu na mungu awabariki..
 
Pole mkubwa......ngoja wataalam watakuzunguki hapa bila shaka.
 

Mkuu hebu weka picha tuone...
Ila wanaweza wakawa wamebanana nafasi ikawafanya wasikue vizuri,

Feeders chache so wanaokula ni wachache wenye nguvu..

Unawapunja chakula..Au wana minyoo.

Wanapigwa na baridi,upepo hivyo kuwafanya wasiwe comfortable kula vizuri..

Vifaranga wakati mwingine vinaweza vikawa vibaya tokea vilipototolewa kiwandani...So hakuna namna.

NB; Kachukue mtaalamu wa karibu atembelee unapofugia anaweza akawa na jibu sahihi zaidi.
 
Daah arafu mtaji umekopa daah ajira nayo ngumu daah
 
Kuna sababu nyingi zinaweza kufanya kuku wadumae.
1. Aina ya vifaranga wenyewe, kuna wengine hawakui vizuri hata ukiwalisha vipi.
2. Chakula kama hakina mchanganyiko mzuri hata kama ni cha kununua si cha kutengeneza inaweza kuleta hali kama hiyo.
3. Hali ya hewa hasa baridi mara nyingi inawafanya kuku wasiwe confortable.
 

nashukuru mkuuu kwa ushauri nafikir ilikuwa hybrid mbaya lakin wanaendelea vizur kuna jamaaa atakuja kuwachukua kesho
 

nashukuru mkuuu wamebadilika jumamosi watachukuliwa mungu akubaliki
 
nashukuru mkuuu wamefanikiwa kubadilika
 
Onana na mtaalamu wa kuku awaangalie kwanza na umweleze historia nzima vingine nasita kushauri bila kuwaona.
 
your case is very broad..!nakushauri nafuta doctor kama mdau alivyosema hapo juu aende sehemu ya tukio,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…