Kuku wangu wanashindwa kutotosoa mayai msaada nifanyaje?

mumuma

Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
56
Reaction score
154
Ninamradi Wa kufuga Kuku Wa kienyeji,tatizo kila wanapotaga hawatotosoe mayai yote,mfano unakuta ametaga mayai 10 akija kutotosoa labda vifaranga 2 au 3,nanikijaribu kuyapasua yaliyobaki nayakuta na vifaranga,Na nitajuaje yai lenye kifaranga ndani na lisiro na kifanga pindi Kuku anapokuwa ametoka kulitaga?
 
Weka chumvi kwenye chombo wanachotumia kuatamia pindi tu wanapoanza kuatamia.
 
Kuna haya mambo matatu ukiyaweka sawa hilo tatizo litaisha

1)weka kiota cha kuatamia katika hari nzuri ili akilalia mayai yapate joto vizuri.

2)yawekee alama hayo mayai anayolalia ili kuepuka kuchanganya huwenda kaanza kulalia mwingine akaja kutaga baadaye pale pale anapolalia mwenzie na ndio hayo unakuta vitoto vilikuwa havijakamilika kutotolewa

3)usiruhusu kuku wasio atamia kwenda kucheza kwenye mayai wakiparua na kutingisha yai lenye wanaharibu.
 
Nmechelewa kuuona huu uzi lkn nachangia tu kwa matumizi ya baadae. Kulingana na uzoefu wangu kuku kutotoa vifaranga wachache inaletwa na mambo yafuatayo:
1. Ubora wa viota
Nitaleta kesho maelezo ya size ya kiota

2. Utulivu wa Kuku
Kiota kiwe sehem tulivu na iliyojificha. Pia hakikisha hakuna viroboto au wadudu watakao kuwa wanawasumbua Kuku wanaoatamia. Nyunyizia dawa za unga za kuua viroboto pia jitahid kuweka viota eneo tofauti na lile Kuku wengine wanalala au kushinda

3. Ubora wa Mayai
Yawe bora na yasiyokaa siku nying baada ya kutagwa,unashauriwa yasizidi siku 14

4. Idadi ya Mayai yaatamiwayo ktk kiota
Usiweke Mayai meeengi kwa Kuku mmoja kuatamia,wastani ni 10 - 12 kwa Kuku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…