Kuku

Jocasta

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
474
Reaction score
595
Kuku wangu wanatoa kinyesi cheupe kama chokaa, ni dalili ya ugonjwa gani na nitumie dawa gani
 
Salmonellosis ambayo yaweza kuwa fowl typhoid au fowl paratyphoid...

Dawa nzuri wape amprolium au dawa yoyote ya sulfur watakuwa sawa..
Mkuu za kitambo!
Samahani natoka nje ya mada kidogo!
Hivi ni kweli utotoreshaji wa mayai kwa incubator unaaridhiriwa na umbali!

Kuna mtu ameniambia hivo kwamba Eti ukisafirisha kiini kinajichanganya ko haliwezi kutotolewa!
Hili ni kweli?
 
Salmonellosis ambayo yaweza kuwa fowl typhoid au fowl paratyphoid...

Dawa nzuri wape amprolium au dawa yoyote ya sulfur watakuwa sawa..
Nakataa Salmonellosis hawanyi mavi meupe. Amesema wanakunya sio kuharisha sawa??
 
Mkuu za kitambo!
Samahani natoka nje ya mada kidogo!
Hivi ni kweli utotoreshaji wa mayai kwa incubator unaaridhiriwa na umbali!

Kuna mtu ameniambia hivo kwamba Eti ukisafirisha kiini kinajichanganya ko haliwezi kutotolewa!
Hili ni kweli?

Kwema mkuu, kwa ufupi tu hakuna athari yoyote itakayopelekea mayai kutokuanguliwa cha msingi tu ni kuzingatia kanuni zote za utotoleshaji...

Kama umeingia kwenye industry hiyo naweza kukuwezesha na document nzuri tu ambayo itakuongoza vyema ili kuepuka kupoteza mayai katika incubator yako....
 
Daaaa asante sana Mkuu! Nadhani unakumbuka kipindi nilikua nakuuliza maswali mengi sana kwenye ule Uzi wako!

Kiukweli umekua msaada Mkubwa sana kwangu mpaka sasa wale kuku (sasso) wanataga ingawa Sio wengi sana ila nashukuru kidogo kinachopatikana kinalisha wao wenyewe na mifugo mingine(nguruwe)

Kwanini nmekuuliza hivo?
Kuna mteja alikuja kununua mayai akaenda kutotoresha akamwambia yametotolewa yote mda kidogo tena akabadisha eti sikuangalia vizuri yametotolewa machache!
Tatizo nini!
Anasema ukisafirisha eti kiini kinachanganyika Kwahiyo hayatotolewi!

Binafsi nmehisi huyu mwenye mashine amempiga panga mteja wangu, maana Kuna wengine wanachukua kwenda kutotoresha kwenye kuku wao wa kienyeji na yanatoka vizuri kabisa na najitahidi sana kufuata ile formula ulinipa na kuwapa mboga ambayo nalima mwenyewe!

Samahani kwa maelezo marefu!
Ingawa sijaanza kutotolesha ila naomba kama hutojali nisaidie hiyo document niendelee kujifua maana natamani niupate ujuzi huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…