Kukuku Hadija yule.. kwako wapi?

kula mbakishie baba
namtafuta mke wangu, namtafuta mke wangu hapa hayupo
hii nayo nilikuwa naipenda kwa maana inakufanya uwe tayari tayari kukimbia.

Kuna mwingine tulikuwa tunachora mduara halafu tunakata vipande kama vile pie chart kila mmoja wetu anachagua kipande na kukipa jina la mji ama nchi anayopenda inakuwa kama ndio ID yake halafu kunakuwa na mtu mwenye mpira hapo inahesabiwa moja mpaka tatu inabidi uwe umeshaingia kwenye kipande chako.

Huu mchezo niliupenda sana kwa sababu ulikuwa njia moja wapo yakutufundisha jografia,ilikuwa kama mashindano fulani ya nani anajua miji na nchi nyingi zaidi ya wengine.
 
Jamni nilikuwa napenda sna kuruka kamba na shake rede ulikuwa unaitwa
 
Ukuti ukuti, wa meme wa meme......

Dori dori, dori sambwela...........

Rede ya wote jigijaaa, kama hutaki sambaa.....
 
Mimi nilikuwa nacheza sana mchezo wa harusi..
mimi nilikuwa bwana harusi.acha tu.......
 
You tell one to guess your age, hii michezo ilikuwa inaendana na 'generation' au 'cohorts' fulani.
 
Niulize niulize ehhh.....
Siku uliyokuja uliyokuja uliyokuja,
Ulivaa nguo gani nguo gani nguo gani:

Nilivaa Tinaboo,
Juu Shati Mtumba,
Chini Raba Mtoni,
Na chupi ya kijani: (hapa probably VIP, ikikatika inapanda kifuani)
Muone Alimasi kwa midundiko,
Anavyolisakata Super Bomboka,
................. Mbeleni Nimesahau (mchezo wa kuruka na kamba).

Looo, huo wa piga magoti nilikuwa nauwaza mwezi uliopita. Hadi leo unanikumbusha Sister wangu wa Mibono (Kiloleli/Enzi hizo Langwa) aliyekuja Sikonge na kutufundisha huo wimbo.
 
Mimi enzi hizo nilipenda sana kwenda kucheza mchezo wa kukalia Kibao tulichoweka Bearings "zilizotumika" katika Jiwe la Gangilonga Iringa... Ama kwa hakika ulikuwa mchezo hatari sana... LOL...
 


hapo nilipo pakaza nyekundu ni kwa wale walioishi na kukulia mbeya miaka ya sabini na themanini
 
Ukuti Ukuti .....ahahaha wamchechema ahaha.. u made my day guys
 
kombolela, we acha tu!
Kula mbakishie baba sijaona mtu akizungumzia....mchezo ulikuwa wa hatari ule...kuna wakati nilipokea kichapo baada ya kudondosha kijiti !! sitasahau...
 
The Following 5 Users Say Thank You to Mzee Mwanakijiji For This Useful Post: Katavi (25th March 2010), Qsm (26th March 2010), Shadow (Today), Sikonge (Today), The Boss (26th March 2010)

Nyie naona mlikuwa manpenda sana michezi hii.....
mie napenda ukuti ukuti wa mnazi wa mnazi ila naona miaka yetu ya 60 nyie hamkuucheza
 
Hii michezo ilisaidia sana kwenye makuzi ya watoto, kiakili na kimwili...! Inatakiwa kwa kizazi hiki wataalam wa uandishi wafanye jitihada za kuihuisha hii michezo kwa kuiweka kwenye vitabu ili kizazi hadi kizazi waweze kuicheza ili isipotee kabisa... wakati ni huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…