SoC01 Kukumbushia Ahadi Za Serikali Ni Sehemu Ya Maendeleo Ya Jamii Yetu

SoC01 Kukumbushia Ahadi Za Serikali Ni Sehemu Ya Maendeleo Ya Jamii Yetu

Stories of Change - 2021 Competition

Abuunuuman

Member
Joined
Sep 11, 2021
Posts
20
Reaction score
29
Jamii yenye ukamilifu wa huduma ni ile inayojitosheleza kupata huduma zote za msingi zinazohitajika Kila siku.

Bahati mbaya sana iliyopo ni kukosekana Kwa baadhi ya huduma za msingi katika jamii yetu ya watanzania wengi na hata huduma zinazopatikana hazikidhi mahitaji kwa ukamilifu.

Ili baadhi ya huduma ziwepo kunalazimu uwepo wa fedha ya kupata huduma kama za maji na umeme Pamoja na Kodi za pango na chakula.

Kutokana na ukosefu wa hizi huduma Kwa watu viongozi wanalazimika kuweka ahadi ambazo uwezo wa kutekelezeka unakuwa ni mgumu Kwa muonekano na hata kutoweka Kwa Imani ya jamii Kwa viongozi wao Hadi pale watakapo shuhudia Kwa macho kuwa imetekelezwa.

Miongoni mwa ahadi zilizotolewa na viongozi wetu ni suala la ongezeko la mishahara kwa watumishi wa umma pindi ifikapo mwaka 2022 mwezi mei ambapo mishahara hiyo ndio chanzo kikuu Kwa watumishi wa umma kupata pesa zitakazo wawezesha kulipia gharama za huduma za msingi kwao na familia zao.

Maslahi ya watumishi wa umma kuboreshwa ni ahadi kuu ya viongozi wetu Kila inapofikia kipindi Cha kuwachagua kwa kura zetu watuongoze lakini utekelezwaji wake umechukua muda Hadi sasa kutoka ilipotolewa na viongozi wetu waliopita.

Ni jambo jema kukumbushia ahadi tulizoahidiwa na viongozi Ili kuepusha lawama kwao ikiwa hazijatekelezwa kwani lawama ni majuto na majuto ni mjukuu.

Kutoka ahadi ya kupandishwa mishahara Kwa watumishi ilipotolewa sasa ni miezi nane imebaki Kufika muda wa kutekelezeka.

Ahadi nyengine zilizotolewa Kwa jamii ni upatikanaji wa uhakika wa Huduma ya umeme Kwa gharama nafuu.

Nikweli gharama ya kuunganisha umeme Kwa mteja mpya imepunguzwa lakini kumewekwa tozo katika umeme ambazo hazikuwepo hapo kabla. Huku huduma ya umeme ikiendelea kukatika Kwa baadhi ya maeneo ikiwemo nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Ahadi ni nyingi zilizotolewa na viongozi sasa ni wajibu wetu kuwakumbusha kama wajibu wetu wa msingi Kwa hali zetu.

Wito wangu Kwa jamii ni kuwahamasisha kuwajibika katika kuzalisha na viongozi wetu wawajibike katika kutimiza ahadi zao Kwa wakati na weledi kwani maendeleo huletwa Kwa ushirikiano mzuri kati ya jamii ya raia wa kawaida na viongozi.

Natumaini neema ya maslahi ya watumishi wa umma kuboreshwa kama ilivyoahidi.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom