Kukuza mtandao na kuwa waaminifu kutatuepusha na madhila ya tozo mpya ya CCM

Kukuza mtandao na kuwa waaminifu kutatuepusha na madhila ya tozo mpya ya CCM

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Ndugu zangu tupo vitani kwa Sasa, Vita hii ni Kati ya watawala wanaolishwa na Kodi zetu dhidi ya watawaliwa. Familia chache zinazotawala nchi hii zimetuletea Kodi kubwa pamoja na tozo huku wakijinadi kwamba TUTAZOEA TU.

Hatuna budi kushikamana na kupeana mbinu zakushinda Vita hii, nawaletea mbinu kuu tatu zakuepuka tozo za simu
1. Tuepuke kwa namna yoyote kutuma pesa sehemu ambayo tunaweza kufika kwa miguu au kwa usafiri wenye bei nafuu. Mfano. Siyo tija kutuma pesa kutoka tegeta kwenda Kariakoo wakati ungeweza kwenda au kumtuma mtu zikafika.

2. Tujenge mtandao wa marafiki wa makundi yote kwenye jamii huku tukikuza uaminifu. Wafanyakazi lazima mjitenegenezee network na wafanyabiashara kiasi kwamba unaweza kuelekeza familia au ndugu yako apewe huduma sehemu yoyote bila kulipia cash kwa wakati huo ambao upo mbali na eneo la huduma. Familia ipo mwanza inahitaji friji, zungumza na muuza friji Dar akuelekeze sehemu ya kwenda kuchukua friji Kisha lipelekwe nyumbani then fanya malipo ukiwa Dar.

3. Lipa kwa mkupuo pale inapowezekana ikiwemo kutuma pesa za familia mara moja then mtoaji azitoe na kuzipeleka kwa wanafamilia. Tabia yakutuma pesa sehemu moja mfano kijijini ukamtumia kila mtu kiasi chake naomba ife. Mtafute ndugu mwaminifu au wakala wa karibu na nyumbani mtumie Kama floti then yeye awape ndugu cash.

Hatupingi kutoa tozo hii ila uwezo wetu kiuchumi ni mdogo sana kuweza kulipa tozo ya laki kwa mwezi kulingana na transaction. Mfanya biashara mwenye mtaji wa milioni kumi akitumia njia ya pesa za mtandao kulipa na kulipwa anaweza akajikuta ametumia laki tano Kama tozo kwa mwezi kulingana na miamala anayofanya. Mhe. Wazir yeye Hana muda wakufanya utafiti maana analipiwa kila kitu.

Mwisho nimshukuru Shigongo kwa kueleza wazi kwamba lengo la tozo hizi nikuzuia uchumi usiporomoke, ila nimjulishe kwamba Sasa hivi ndo uchumi unakwenda kuporomoka maana mitandao ya simu inakwenda kupoteza watuma fedha na hivyo waajiriwa wa sekta hii wanarudi kitaa kuongeza watu wasio na ajira.
 
Shigingi amesomea uchumi?
Madelu ameshindwa kujua faida na hasara kaingia mazima.

Huko kigoma nimemsikia VP
Anasema "Mimi nilisoma kwasababu mama alikuwa anauza miwa na machungwa"
Hivyo na ninyi mfanye vivyo hivyo ili watoto wenu wasome (sikumuelewa kabisa kwa karne hii)
Eti watumie mbinu ya mzazi wake enzi hizoo
 
Back
Top Bottom