SoC02 Kukuza na kuendeleza Elimu Tanzania

SoC02 Kukuza na kuendeleza Elimu Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Omari Frank

Member
Joined
Jul 22, 2022
Posts
14
Reaction score
5
Mada kuu: Elimu
Jina la mwandishi: Omary Frank
Manispaa: Morogoro Mjini
Mkoa: Morogoro
Mawasiliano: 0767408787
Email: hamadiomary07@gmail.com

KUHUSU MWANDISHI

Omary Frank ni Mwalimu, Mjasiriamali mdogo, Mkulima na mdau mkubwa wa maendeleo. Pia ni mwanzilishi wa mradi unaojulikana kama (DEVELOPMENT CYCLE) ambao unawaleta pamoja wadau wa maendeleo kutoka kada mbalimbali.

Kazi za mradi huo ni;
  1. Kupeana taarifa mbalimbali kama vile ( Ajira mpya, Ufadhili wa masomo, Mikutano na makongamano ya maendeleo)
  2. Kupeana elimu na uzoefu wa Biashara, Kilimo na Ufugaji
  3. Kutokana na uwepo wa Wanasheria, Maaskari, Walimu, Wataalamu wa Teknolojia, Wahandisi, Waandishi wa habari, Wanamichezo, Wasanii, Waigizaji, Wakulima, Wafanya biashara na wadau wengine wengi, Hivyo basi tunapeana msaada wa Kisheria, Kitabibu, Kisayansi na Teknolojia, Elimu, Sanaa, Michezo na mengineyo.
Mradi huu wa maendeleo ulianzishwa rasmi 02/10/2021.

KUKUZA NA KUENDELEZA ELIMU NCHINI

Elimu ni mfumo wa kupeana ujuzi na maarifa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwengine kwa njia mbalimbali ikiwemo mashuleni, Jandoni, Unyagoni, Katika shughuli za kiuchumi kama vile Uvuvi, Uwindaji na Kilimo ambapo elimu husambazwa pale mtu anapofundishwa namna sahihi ya kufanya shughuli hizo kwa ufasaha.

Nchini kwetu Tanzania maendeleo katika kada ya elimu ni makubwa sana ukilinganisha na miaka ya nyuma na hii inachagizwa na sera mbalimbali za elimu kama vile (MATOKEO MAKUBWA SASA (BRN), SHULE ZA SEKONDARI KATIKA KILA KATA, ELIMU BURE KUANZIA MSINGI HADI KIDATO CHA SITA) pamoja na usimamizi mzuri unaofanywa na serikali katika kuboresha miundo mbinu na maslahi ya waalimu mfano ( KUJENGWA KWA MADARASA, MABWENI, MAABARA, KUPANDA MADARAJA KWA WAALIMU na KUONGEZWA KWA MISHAHARA)

Pamoja na maendeleo hayo, Elimu bado ina changamoto kadhaa ambazo zinatakiwa kufanyiwa kazi ili kukuza na kuendeleza kada hiyo kwa hapa nchini kwetu Tanzania. Andiko langu litajikita zaidi katika kueleza mambo ya kufanya kama Taifa ili kukuza na kuendeleza kada ya elimu nchini.

  1. Kudumisha pembe tatu baina ya Wanafunzi, Waalimu na Wazazi. Kuboresha mahusiano katika pembe tatu hii kunachangia kwa kiasi kikubwa sana maendeleo mazuri ya mwanafunzi darasani. Mawasiliano ya karibu baina ya watu hawa huweza kuibua changamoto za mwanafunzi na kufanyiwa kazi mapema kabla hazijaleta athari katika maendeleo yake darasani pia hudumisha nidhamu, Hili linasadiki kuwa umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
  2. Shule za ufundi na masomo ya ujuzi. Serikali inatakiwa iongeze na kusimamia kwa karibu sana shule za ufundi lakini pia masomo ya ujuzi mashuleni kama vile kushona, mapishi, kupamba, urembo, kuchora, kuchonga, umeme na mengineyo. Umuhimu wake ni kwamba vitawasaidia wanafunzi kupata ujuzi ambao utawawezesha kujiajiri baada ya kumaliza shule. Taifa leo hii linashuhuduia kundi kubwa la wahitimu wa vyuo vikuu mitaani ambalo halina ajira na halina uwezo wa kujiajiri, vijana wengi wana elimu bora lakini hawana ujuzi na ndio maana wanapata tabu na wengine wanaishia kujiingiza katika makundi ya vibaka na uhuni. Lakini kama vijana hawa watapatiwa elimu ya ujuzi itawasaidia sana kujiajiri na kumudu gharama za maisha na kulipunguzia Taifa mzigo.
  3. Michezo mashuleni. Serikali inafanya kazi nzuri sana kuhimiza michezo mashuleni, tumeshuhudia UMITASHUMTA imerudi na sasa ni wakati ambao wazazi na waalimu kuiunga mkono serikali katika kuhakikisha michezo inafanyika ipasavyo mashuleni kwasababu michezo hii huibua vipaji, huimarisha afya ya akili na mwili, husaidia kupunguza athari za magonjwa na kuimarisha mahusiano mema baina ya jamii. Watoto wadogo wafundishwe kwa kutumia nyimbo na michezo mingi hii itawasaidia kuelewa na kukariri vitu kwa haraka zaidi.
  4. Jamii kuwalinda wanafunzi kwa kutoa taarifa za ndoa za utotoni, walemavu wanaofichwa ndani na familia zao, watoto wanaofanyishwa kazi badala ya kupelekwa shule na pia kuwapa msaada wa hali na mali watoto kama vile mayatima, wanatoka katika mazingira magumu na wengine wengi ili kuhakikisha wanaata elimu bora na katika mazingira salama na tulivu.
  5. Matumizi ya sayansi na teknolojia mashuleni. Kuweka kompyuta na mifumo ya internet ili wanafunzi waweze kupakua masomo mitandaoni, Hili lifanyike kwa haki na usawa kwamaana shule nyingi za vijijini zimeachwa nyuma sana linapokuja suala la Tehama. Wanafunzi wote nchi nzima wana haki sawa, wanatakiwa kupatiwa elimu bora na yenye viwango ili kuendana na ushindani ulioko kwenye soko la ajira lakini pia kwenda sawa na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.
  6. Kuongezwa kwa miundo mbinu kama vile madarasa, maabara, maktaba, mabweni, ofisi na nyumba za waalimu hususan kwa shule za vijijini ili kuwezesha watoto wengi kupata elimu bora. Pamoja na jitihada zinazoendelea kufanywa na serikali katika kuboresha elimu vijijini lakini bado nguvu kubwa inahitajika, wananchi pia wanatakiwa kuhamasishwa kujitolea kujenga miundo mbinu ili watoto wao wasome mahali pazuri kwa maendeleo yao wenyewe, wazazi wao na jamii zao kwa ujumla.
Kwa ujumla, Hayo ni baadhi tu ya mambo mimi kama mdau katika kada ya elimu nadhani tunahitaji kuyafanyia kazi ili kukuza na kuendeleza kada hii nchini. Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi pamoja na wananchi pia imekua ikijitahidi sana lakini bado nguvu kubwa inahitajika ili tuweze kufika mahali pazuri zaidi.

Ninatanguliza shukrani kwa Mwenyezi Mungu, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Uongozi mzima wa Jamii Forums, Wanajamii Forums, Wadau wote wa maendeleo kutoka jukwaani (Development Cycle). Itifaki imezingatiwa.

Tupo pamoja katika ujenzi wa Taifa.

Viva Tanzania, Viva JamiiForums.
 
Upvote 4
tofaut na kukndoa ujinga kichwan elimu ya Tanzania haina faida yyte but nikupongeze maana wewe humepata kazi but hungeangalia vitu vingine tofauti na elimu maana sisi hatuon faida zake
 
Faida zipo kaka, ndio maana tunasisitiza serikali iimarishe shule za ufundi, kuibua vipaji mashuleni, kuimarisha matumizi ya tehama n.k. Vyote hivi ni sehemu ya elimu na vina mchango mkubwa sana katika maisha ya kujiajiri na hata kuajiriwa. Ahsante🙏
 
Ni kweli vipo lakini kama ulivyosema kuna mambo mengine mengi yanatakiwa kupewa nguvu kama hizo tafiti ulizosema pia kutia mkazo kwenye hizo shule na vyuo, kutia mkazo kwenye masomo ya vocational skills mashuleni kama vile mapishi, urembo, upambaji n.k sisi ndio wakupaza sauti na kushinikiza ili ipatikane elimu yenye tija kwa vijana wetu. Naamini safari bado ni ndefu lakini tutafika tu kaka. 🙏
 
Back
Top Bottom