Kukwama kwa miradi mikubwa ya NHC kunaumiza, kunaliza kunasikitisha sana. Ni wazi Nehemia Mchechu alikuwa bora? kwanini Lukuvi na Jenista bado wapo?

Mwendazake hakupenda kuona mtu mwingine anasifiwa wakati yeye yupo na ameharibu mashirika mengi sana ya umma kwa ubinafsi wake.
 
hakika
 
lakini pamoja na yote alilifanya shirika likawa na nguvu sana
 
Kuliokoa shirika inabidi miradi yake imalizwe
 
Haya, baada ya kumuondoa mpiga dili, Magufuli alivyomuweka jamaa yake asiyempiga dili, maendeleo yako wapi hata nusu ya yale aliyokuwa anafanya msechu?
 
Miradi ikamilishwe,huku mchawi akiendelea kutafutwa amalizwe.
 
Real estate sasa iv ime fulia sanaaa mfano tu kuna jengo pale la pembeni moroco sijui lina floor kama 7 iv hamna wapangaji ...maofisi yana fungwa
Ofisi za nini kwenye zama za teknohama..
Watu wafungua ofisi kwenye laptop na waajiriwa wote wana laptop kwisha mchezo....
Wazungu wenyewe ulaya wanalia na magorofa yao hamna watu wanapanga kufungua ofisi....
 
 
NHC ya Mchechu ilikuwa inalenga wenye hela ndefu tu. Nyumba zinauzwa Tshs. milioni 250 hadi milioni 360!

Ni vema kibiashara kujenga nyumba za bei mbaya kwa ajili ya wenye hela, lakini wangejigawa wakajenga na nyumba za sio zaidi Tshs. milioni 30 kwa ajili ya wananchi wa ngazi ya chini. Na pia Tanzania inahitaji nyumba ambazo mtu anaweza akamudu kuimiliki kwa malipo ya pesa sawa na kodi ya pango kila mwezi. Yaani mtu alipe Tshs. 100,000/- kwa mwezi, 200,000/- kwa mwezi au 300,000/- mpaka amalize bei ya nyumba. Hata akipewa miaka 20 au 30 kulipa sio mbaya.

Mkataba uwe mkali kuwa akichelewesha malipo kwa miezi kadhaa (miwili au mitatu sio mbaya) nyumba yake inawekwa sokoni kwenye mnada ambapo mnunuzi atatakiwa kulipa kwa mkupuo pesa yote ambayo mkazi huyo ameshalipa mpaka hapo aliposhindwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…