Elections 2010 Kula CCM, kura CHADEMA

Elections 2010 Kula CCM, kura CHADEMA

Hii imetulia, wananchi wakielimishwa kuwa ukila hivyo vi takrima vyao sio lazima uwape kura kwa sababu kura ni siri yako na maamuzi ni yako mwenyewe, CCM watachemsha ,kwani kule vijijini wanawadanganya na kuwatisha kuwa ole wenu usipigie ccm maana tutajua.
 
Mimi hii nimeipenda. Wadau wanaoweza kujitolea kutengenza vipeperushi vya kutosha venye ujumbe huu wanaombwa wafanye hivyo.
 
poa mku, tupe mahali pa kuanzia...

Naamini humu ndani kuna madisigner wa majarida na vipeperushi vya aina nyingi. Wanaombwa kujitokeza na kutuyambia kwa mfano kipeperushi cha rangi chenye ukubwa wa 7" x 5" kinaweza kugarimu bei gani. Baada ya hapo wengine tujitolee kumlipa kwa idadi yoyote kama 100,500,...nk. Atuambie namna atakavyopenda afikishiwe hela, na kutuhakikishia kuwa atadeliver kwa kadri ya makubaliano. Anaweza pia kubandika sample ya vipeperushi vyake kwa maoni zaidi ya wadau.
 
any comments please...

Hii kauli mbiu aliitumia Mbunge wa Moshi Mjini Ndesamburo (aka Ndesa Pesa) kumbwagia Shem wake na Ben Nkapa (wakati hajastaafu ukiranja Mkuu wa inji hii) aitwaye Mama Minde: Kula kwa Mama Minde Kura kwa Ndesamburu na kweli jamaa wakafanya hivyo
 
Hii kauli mbiu aliitumia Mbunge wa Moshi Mjini Ndesamburo (aka Ndesa Pesa) kumbwagia Shem wake na Ben Nkapa (wakati hajastaafu ukiranja Mkuu wa inji hii) aitwaye Mama Minde: Kula kwa Mama Minde Kura kwa Ndesamburu na kweli jamaa wakafanya hivyo


Hii nafikiri imetulia kabisa, na inafaa sana, nafikiri inatakiwa kufikiishwa kwenye kamati ya ushindi mapema iwezekanavo
 
itabidi hii ifikishwe kwenye baraza la vijana BAVICHA ili iangaliwe kama ianaweza kuwa kauli mbiu yetu au sub kauli mbiu hasa vijijini, nafikiri kama Mnyika yumo humu kwenye jamvi leo aipitie hii na wadau wengine watoe mawazo yao
 
KULA CCM, KURA CHADEMA.

Imekaa vizuri sana--------------CHADEMA HUREEEEEEEEEEEEEEEE, USHINDI DAIMA
 
Kimtindo au kiuhalisia kwa sasa hii ingekuwa imekaa vema, maana hata leo asubuhi napita maeneo ya jiji nakuta watu wamejihimu asubuuuhi na nguo kibao za CCM, utafikiri wanaipenda. Kumbe ni hizo pesa zetu sisi tunazolipa VAt, na kodi zingine wanatafuna

Wao hawana kosa kuzitafuna ila kura wampe mwingine naye aanze kuwapa hizo mapemaaaa siyo kila baada ya miaka mitano.
Du!, Watu wangepewa hii tungefika mbali sana.
 
Akili kichwani umenena mkuu, hili ni wazo babu kubwa. Naungana na wadau wenye mapenzi mema na nchi yetu limetulia. Here we go "Kula ccm KURA CHADEMA". Cha muhimu ujumbe ufikishwe kila mahali nchini. Kila mtu kwa nafasi yake, mwenye uchungu na hii nchi kwa ajili ya vizazi vijavyo afikishe ujumbe huu kuinusuru!! Go Dr. Slaa Goooooooooo!!!
 
Back
Top Bottom