Hivi ni gr6 thinkers au sinkers maana jamaa kasema ameoa, watu mmekomaa ooh aziniye sijui na nani.......aaaargh muwe mnasoma vizuri kwanza bana.
Me pia nimeshangazwa na hawa great thinkers! Mwenzenu amesema ameoa, watu wanasema anazini. Nani kasema miaka 24 ni mtoto mdogo? Anaweza kuwa mdogo sana kiumri kwako, lakini ni mtu mzima mwenye akili zake!
Kama mtu ameuliza swali, jibu, sio kuwa off point. Me mbona mama yangu aliolewa na miaka 20? Ni mpango wa maisha tu. Wale wanaosema asihangaike na mapenzi, akazane na elimu, kwani yeye amesema hasomi? Tuache kupayuka.
Watu tunadhani kuwa ukubwa wa umri ndio umezo wa kufikiria. Kama ingelikua ni kweli, basi msamiati wa KUBWA JINGA usingekuwepo.
Kwa upande wangu, Pape ameonyesha uwezo mzuri tu wa kufikiri, kuliko wengi tu waliotupa madongo bila kuelewa wanajibu nini.
Bottom line:
Hakuna madhara ya kiafya, ladba kama yatasababishwa na matatizo mengine nje ya hapo. Kama ni mkeo mridhishe, achana nao hao wanaopayuka. Na kama unaona hauko katika nafasi ya kuwa na mtoto sasa hivi, ni vyema usubiri.
I like it, umeonyesha una plan ya maisha.