Anayekula ndotoni,hashibi asilaniSwali linanitatiza, jawabu natafutia,
Nimebaki ninawaza, nani atanipatia,
Sina wa kunijuza, bora kuwaulizia,
Mtu akila ndotoni, huamka ameshiba?
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Vuvuzela Matata)
Mhhhhhhhh! Kwa jinsi ulivyo mtu wa hoja kali, napata shida kidogo kujibu swali hili. Sijajua kama huku kula ni kula kwa kawaida au kuna zaidi ya ujumbe ambao ungependa sisi tukujuze. Nachelea kufananisha na ule wimbo wa taarabu wa mdudu kaingiaje ndani ya kokwa la embe. Ngoja nifikiri kidogo, maana waswahili husema, anapoongea profesa, ni vyema waungwana mfikirie maana hatutegemei profesa aongee kitu kwa upeo wa kawaida.Swali linanitatiza, jawabu natafutia,
Nimebaki ninawaza, nani atanipatia,
Sina wa kunijuza, bora kuwaulizia,
Mtu akila ndotoni, huamka ameshiba?
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Vuvuzela Matata)
Swali linanitatiza, jawabu natafutia,
Nimebaki ninawaza, nani atanipatia,
Sina wa kunijuza, bora kuwaulizia,
Mtu akila ndotoni, huamka ameshiba?
Swali linanitatiza, jawabu natafutia,
Nimebaki ninawaza, nani atanipatia,
Sina wa kunijuza, bora kuwaulizia,
Mtu akila ndotoni, huamka ameshiba?
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji a.k.a Vuvuzela Matata)
Ni bure watatizika, kwa swali ulouliza
chakula huwa chalika, tena wengine husaza
Kipikwe kikapikika, mlaji kukimaliza
yategemea mlaji, kula ndotoni washiba.
Kwa alaye bakulini, au alaye kwenye mwiko
kushiba ni majinuni, atashiba mwenye mwiko
Hupunjwa wa bakulini, kushiba kwake ni mwiko
Atashiba mwenye mwiko, na sahani kuchafua.
Mwanakijiji hujambo? umelishwa ndotoni nini baba?
Mj1 mwenye bakuli ndo hufaidi, huchagua kivuli apate kufaidi,tena kelele apiga pilipili ikinoga,mwenye bakuli afaidi mchuzi pia na ujira..mwenye upawa huonja mchuzi mwenye bakuli kushiba ndo jadi...m'kijiji ashibaye ndotoni ndiye mlaji wa ukweli...tena atakula..