Runner
Member
- Feb 7, 2011
- 85
- 13
Habari wana JF,Wapendwa naomba msaada wenu kwenye hili tatizo linalonitatiza,imekuwa ni wiki sasa huwa napatwa na usingizi mzito sana ifikapo saa nne asubuhi,yaani iwe nimewahi kulala usiku au nimechelewa lakini ikifika muda huo kwa kweli huwa napata shida sana hata kufanyakazi,na si saa nne tu bali na saa kumi jioni.Katika nyakati hizo mbili kweli jamani huwa nateseka sana na huo usingizi mzito,lakini ikishapita muda huo usingizi unapotea kabisa kama vile sikuwa na huo usingizi.Naomba mwenye ufahamu juu ya hili anipe elimu,ni tatizo gani?nateseka sana jamani