Tunashukuru sana kwamba hivi sasa bodaboda zimetengeneza ajira kwa vijana wetu wengi.
Lakini jamani, tuwe makini sana sana na sehemu tunazolaza bodaboda hizo au pikipiki zetu baada ya shughuli zetu za kila siku. Moto wake ni hatari sana. Ni kama bomu!
Ilitokea sehemu (singependa kuitaja), jamaa alisafiri akaacha pikipiki sebuleni. Pilikapilika za watoto wakati wa mapishi, ile pikipiki ilishika moto. Sasa mbaya sana kizima moto ilikuwa ni ndoo ya maji!
Daa! Ndugu zangu, nyumba ilikuwa ni ya vigae, kilichobaki ni kuta za tofali tu! Kila kitu kiliungua. Mpaka fremu za milango na madirisha!
Hakuna aliyepoteza maisha, sababu wote walijiwahi nje!