Kulazimisha kulipa bili ya umeme wa Luku pamoja na kodi ya jengo ni kiroja

Kulazimisha kulipa bili ya umeme wa Luku pamoja na kodi ya jengo ni kiroja

Shoctopus

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
3,434
Reaction score
1,985
Asalam-alaekoum Wana-JF!

Kama wapo wataalamu wa sheria na haki za binadamu humu ninapenda wanisaidie kudadavua mada ya hapo juu.

Simu yako kwanza ni chombo chako cha mawasiliano binafsi.

Pili unaponunua line yako ya simu unaingia mkataba na kampuni husika kwamba hatatumia line yako kwa masuala mengine yasiyohusiana na madhumuni ya line.

Kwa mfano unaponunua umeme, una hiyari ya kutumia app ya line ya mtandao husika au kwenda kununua TANESCO au kwa wakala.

Unaweza hata kumnunulia LUKU mtu mwingine kwa simu yako. Sijasikia TANESCO wanaweka bili ya maji kwenye mita yao, kama anavyotaka kufanya Mwigulu.

Kwanini Wizara ya Ardhi au TRA ambao ni wakusanyaji wa kodi wasianzishe app za kulipia property tax? Kuna ugumu gani?

Wakifanya hivyo kodi yako ya jengo inaweza kulipwa na mtoto wako au jirani nk kama ilivyo kwenye manunuzi ya LUKU.

DAWASCO kabla ya kuwa DAWASA walikuwa na app yao tulikuwa tunaitumia kucheki bili na kulipia.

Hii ya kulazimisha kulipa bili ya umeme wa LUKU pamoja na kodi ya jengo ni kiroja.


Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Nakuunga mkono kwenye kuishangaa serikali. Tanesco nao watuambie sisi wateja wao kama nao wamebadili malengo yao ya kutuuuzia umeme na kuwa wakusanya Kodi ya majaengo? Niliuliza hapa Tena kwa kumtag waziri mleta mjadala kuwa inakuwaje kwa wale wanaoishi nyumba za serikali, shule, zahanati, hospitali na hata magereza na vituo vya polisi ambao hununua umeme kwa matumizi ya ofisi nao watakatwa Kodi ya jengo ambalo kimsingi ni la serikali? Au Kuna utaratibu mwingine?
Kwanini wizara ya ardhi na majengo isije na account yake ya online itakayotumika kulipa majengo kama ilivyo dawasco na tra? Mh. Lukuvi amka na acha kuwachangisha wapangaji Kodi ya nyumba ilihali wenye nyumba wameshachukua Kodi yao mapema!
 
Ni kama vile unaponunua mafuta ya Petrol au Diesel unalipa na Motor Vehicle hapo hapo...
 
Back
Top Bottom