SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 1,213
- 1,918
Nimekuwa nikifuatilia huu mfumo unaochezwa na Simba sasa wa kuwategemea mabeki wa pembeni waje kutengeneza nafasi kwenye kufanikisha mashambulizi pale na kushuhudia unavyotufelisha kwa sasa. Kwasababu:
Maana kuna muda unawakuta MUTALE, MUKWALA NA BALUA wanakimbia kuelekea kwa mpinzani lakini wamejikusanya sehemu moja na pembeni kwenye FLANKS hakuna mtu, kwahiyo washambuliaji wamejikusanya sehemu moja kiasi kwamba viungo wa kati akina AHOUA wanakosa option za kusambaza mpira na mwishowe tutawaona magalasa.. Na hata pasi zikienda huko pembeni zinaishia kupotezwa tu.
Kwanini kocha asiwaache MUTALE na BALUA wacheze kwenye mapana ya uwanja ambako ndo NAFASI ZAO ASILIA wafanye timu ifunguke iwe na uwanja mpana wa kusamba mpira halafu MUKWALA akae kati na nyuma yake wakae AHOUA kama na AWESU au FERNANDEZ???? Halafu akina ZIMBWE na KAPOMBE wakawa na jukumu kubwa haswa la kuzuia..
WACHEZAJI NDO WANATENGENEZA MFUMO KWA MUDA HUO ULIOPO NA SIYO KULAZIMISHA VITU AMBAVYO HAVIWEZEKANI...
MFANO WAKATI WA KUSHAMBULIA TIMU IKAWA NA MWONEKANO HUU HAPA CHINI SI TUTAUPIGA MWINGIIIII!!!!!
- Zimbwe tokea enzi hizo ni mbahatishaji kwenye kupiga cross sahihi na pasi za mwisho, na hizo cross mara nyingi anajibutulia tu mpira. Amechangia kupoteza mipira mingi ambayo kama ingetumika sahihi ingechangia Simba kufanya vizuri.
- Kapombe amepoteza ufanisi kwenye kusaidia timu kushambulia. Misimu iliyopita alipokuwa kwenye ubora wake aliifanya vizuri sana kutengeneza magoli kwa kupiga cross zenye macho haswa zile "V-PASS" na hata kufunga magoli mfano alipokuwa AZAM FC alifunga magoli mengi kupitia mfumo wa 3-5-2. Lakini kwa sasa Kapombe si yule tena, maana nguvu zinapungua kutokana na umri unavyoenda, ukizingatia kuwa mfumo huo wa kusaidia kwenye kushambulia na kukaba unahitaji utimamu mkubwa wa mwili na misuli yake katika kukimbia kufanikisha matukio yote hayo.
- Kijiri yeye atakupa mibio mingi sana ila kama kawaida yake pasi ya mwisho ni mgogoro mkubwa tena sana.