Kulekea Wiki ya Ustawi wa Jamii Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Nandera E. Mhando ameendesha kikao cha Wamiliki wa Vituo vya Kulelea Watoto Wadogo Mchana, Makao ya Watoto na Nyumba Salama ikiwa ni sehemu ya Maandalizi ya Wiki ya Ustawi wa Jamii itakayofanyika katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama Mkoani Dar Es Salaam kuanzia Agosti 25-30, 2025.