Leo nimebahatika kufika Ofisi ya ATCL Mwanza kwa ajili ya booking. Niliyoyakuta pale haileti hadhi kuwa ile ni ofisi ya ATCL.
Uongozi fuatilieni na muimarishe ofisi ya Mwanza iwe na hadhi kama ofisi ya ATCL.
- Kihadhi kwa kweli ofisi imechoka mbaya. Ofisi haikupakwa rangi kwa kweli muonekano wa nje ni chafu.
- Nilipoingia ndani nimewakuta watumishi watatu. Nimewakuta hawana kazi kabisa mmoja alikuwa anaendelea tu kuchat kwa simu. Sijui ni hali siyo nzuri, wananchi hawana hela mfukoni.
- Mbaya zaidi hawakuwa na uniform inayomtambulisha kuwa huyu ni mtumishi wa ATCL. Kila mmoja alikuwa na sare iliyo tofauti na wenzake hii ina maana kila moja alivaa alivyopenda.
Uongozi fuatilieni na muimarishe ofisi ya Mwanza iwe na hadhi kama ofisi ya ATCL.