Kulikoni timu za mpira toka Kaskazini(Arusha,Manyara na Kilimanjaro)

kiwiko

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
1,341
Reaction score
2,214
Habarini wakuu. Wakati kukiwa na shamra shamra za timu toka mikoa mbalimbali kupanda daraja kwenda ligi kuu upande wa kanda ya kaskazini bado hakuna matumaini ya kupata timu ligi kuu.
Ni misimu kadhaa sasa hakuna timu yoyote inayowakilisha hii mikoa hivo kuwakosesha burudani wapenda soka wa upande huu wa nchi.

Ina maana hawa viongoz wa hii mikoa hawaoni faida za kiuchumi zinazoletwa na ligi?

Tatizo ni nini maana Moshi na Arusha zina viwanja vizuri tu???

Uwanja wa Amri Abeid Arusha


Uwanja wa Ushirika moshi
 
Wachaga hawawezi kuacha kutafuta hela na kwenda kudili na mipira
Kwani wanaocheza mpira wanalipwa mapumbu??? Acha excuse zisizo na kichwa. Tunataka tupate shida ilipo ili wajikwamie kisoka watengeneze mkwanja zaidi
 
Sisi tunatafuta hela kwanza.hayo mambo ya mipira baadaye kama burudani tukishapata hela.
 
Kaskazini ipo vizuri zaidi katika Sanaa.

Mpira siyo kipaumbele kikubwa sana kwao. Si unajua hata China haina Ligi kuu katika Ulimwengu wa soka?. Labda kwa sasa ambapo soka ni issue sana.

Hakuna ulazima wa sote kuwa wanasoka. Wanaocheza wanatosheleza, Labda mpaka matokeo chanya yaonekane. Si unajua Kaskazini wapo kimkakati zaidi?.

Lakini zaidi sana tunahitaji Wahasibu wabobezi, Madaktari bingwa, Wahandisi makini, Wanasheria hodari na orodha inaendelea..Wanasoka ni wengi mno Nchini.
 
Kwani wanaocheza mpira wanalipwa mapumbu??? Acha excuse zisizo na kichwa. Tunataka tupate shida ilipo ili wajikwamie kisoka watengeneze mkwanja zaidi
Hebu tuambie Shinyanga wana timu VPL nadhani. Wameshatengeneza mkwanja kiasi gani hadi sasa? Kuna economic impact yoyote kwa uchumi wa Shinyanga kutokana na kuwepo hiyo timu? Maana Dar kuna Simba na Yanga lakini hamna cha maana wanachofanya zaidi ya kulogana kila wakikutana na kuweka kambi Pemba ili wajizindike
 
Fursa za kiuchumi zipo aisee labda kama tutakua wavivu wa kufikiri ndo hatutaziona.
 
Tanga coast union nayo ni ya kusini
Ndo maana sijaitaja kwenye mabano so mikoa tajwa inabidi iige mfano wa coastal union ya Tanga. Hongera kwa viongozi wa Tanga wakiongozwa na Mh. Waziri Ummy mwalimu kwa juhudi walizofanya. Wameona mbali. Njombe mji wanachezea mechi za ligi kwenye uwanja wa shule hivo ni aibu kwa mikoa mikongwe kama Arusha na Moshi kukosa timu ligi kuu.
 
Vijana huku kumkuta anavaa jezi kila jioni kwenda uwanjani ni mbinde hizo mambo nimeona tanga sio Kilimanjaro
 
Singida utd hakuna hata mchezaji mmoja mzawa wa singida

Yanga sc kikosi cha kwanza mzawa ajibu pekee yake

Kagera sugar hivyo hivyo

Nk nk


Bado sijaona hoja mpaka hapo


Hio mikoa ya kaskazini ikifika weekend wanafungulia radio kufuatilia matokeo za yanga na simba na wanatamani sana weekend waingia viwanjani kupata burudani ila ndio hivyo tu

Viongozi wa vyama vya soka huko hawana muelekeo
 
Vijana huku kumkuta anavaa jezi kila jioni kwenda uwanjani ni mbinde hizo mambo nimeona tanga sio Kilimanjaro
Kwani singida utd kuna mchezaji wa kutoka singida mule

Kagera sugar ?

Yanga kuna mchezaji wa kutoka dar labda ajibu pekee ila wengine foreigners

Bado hujatoa hoja ,viongozi wa vyama vya soka huko wanakula mishahara ya bure


Vilabu vinacheza daraja ya 2 ila hazipewi sapoti
 
Angalia mikoa inayofanya vibaya kwenye matokeo ya Msingi na Kidato cha nne ndiyo inaongoza kutoa Wachezaji na Wasanii.
Wacheza mpira wengi ni watu ambao shule hawakuwa vizuri .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…