Kulikuwa na sababu gani haswa ambazo zilipelekea Rais Mstaafu Kikwete kuweka jiwe la msingi Bandari ya Bagamoyo kabla ya Mikataba kusainiwa?

Kulikuwa na sababu gani haswa ambazo zilipelekea Rais Mstaafu Kikwete kuweka jiwe la msingi Bandari ya Bagamoyo kabla ya Mikataba kusainiwa?

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463
Ilikuwa Oktoba 16, 2015 pale Bagamoyo ambapo Rais wa wakatiuo Jakaya Mrisho Kikwete aliweka jiwe la msingi kuashiria ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo unaanza rasmi huku akiwa Mkurugenzi wa kampuni itakayojenga Bandari hiyo.

Zoezi ilo lilifanyika siku 8 tu kabla ya Uchaguzi mkuu ambapo Mh Jakaya Kikwete alikuwa amalize mdawake wa utumishi wa uRais.

Muda ulisonga Jakaya Kikwete akamaliza mdawake wa uongozi wa nchi akapatikana mrithi wake ambae alikuwa Mh John Pombe Joseph Magufuli ambapo kwa upande wake aliuelezea mradi wa Bagamoyo kuwa ulikuwa na Masharti ambayo yangeifirisi nchi huko mbeleni, ufafanuzi huu pia ulitolewa na Engineer Kakoko ambae alikuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania bapo kwasasa uteuzi wake ulishatenguliwa na pia Bwana Mkinga ambae alikuwa mjumbe wa Bodi ya TPA mnamo May 05, 2019 akihojiwa na Star Tv pia alipinga masharti yaliyokuwa waliyoweka Wachina ili kutekeleza mradi uo.



Mjumbe wa Bodi ya TPA Renatus Mkinga alifariki dunia May 25 2021 kabla ya kuvunjwa kwa Bodi ya Tasac na Mh Samia Suluhu Hassan.

Kwasasa Mh Samia Suluhu Hassan alilielezea Taifa Mazungumzo ya Mradi wa Bagamoyo yataanza tena mara baada ya kusimama kipindi cha mtangulizi wake Hayati Magufuli aliefariki March 17 202, huku akiahidi kuanza tena upya kabisa kama kama hakukuwa na majadiliano yoyote katika awamu ya 5, Mh samia kuhusu ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwake anaanza alipoishia Jakaya Kikwete na sipo alipoishia John Pombe Magufuli.

Waziri Mwambe ambae ni Waziri wa Uwekezaji alilieleazea taifa kuwa hakukuwa na mkataba wowote uliowah kusainiwa juu ya ujenzi wa Bandari iyo ya Bagamoyo kitu ambacho kimezua minong'ono ya watu wakijiuliza ilikuwaje kuanzisha mradi pasi kuwa na mkataba kipindi cha awamu ya nne?

Kulikuwa uwalaka gani haswa kama hakukuwa na mkataba?

Je, Mchina angejenga Bandari bila Mkataba? Ikumbukwe kuwa utaratibu unatakiwa Mkataba usainiwe ndipo jiwe la msingi lije kuwekwa ambapo baada ya kusainiwa mkataba mkabdarasi anatakiwa apewe miezi 6 yakuleta mitambo yake ili aanze ujenzi, na utaratibu ulivyo ukiweka jiwe la msingi ni kiashiria mradi unaanza rasmi sasa na ni sawa mkandarasi umemkabidhi eneo lake.

Watanzania tutamkumbuka na kumlilia nani juu ya sarakasi za Bandari ya Bagamoyo?

Screenshot_2021-12-03-12-26-54-49.jpg
Screenshot_2021-12-03-12-26-58-10.jpg
Screenshot_2021-12-03-12-27-07-60.jpg
2787792_TPA.jpg
 
Swali langu ni moja tu, zaidi ya wanasiasa, je nchi hii kuna vyombo vinavyoangalia na ku define maslahi ya taifa? So mwanasiasa mmoja na kikundi chake wakiamua jambo nchi nzima inaingia kwenye shimo hata kama jambo hilo halina maslahi kwa taifa? Ni swali mwenye (we) akili wanisaidie kujibu.
 
Moderator Naomba unibadilishie kichwa cha habari na kisomeke "Kulikuwa na uharaka gani kuweka jiwe la msingi Bandari ya Bagamoyo kabla ya Mikataba kusainiwa?"
 
Usichanganywe na wanasiasa!!

Waziri naye aliongea hata hajui aliongea nini!!

Viongozi wetu kila mtu na lake, hakuna wa kumuamini si heri wakaweka wazi kuhusu huo mkataba.

Magufuli alisema yake , wananchi hawakuonyeshwa mkataba.

Waziri naye leo kasema yake ati hakuna mkataba uliosaniwa. Wakati video clips zinaonyesha enzi Kikwete anasaini na watu walishuhudia.

Yaani sarakasi utafikiri nchi hii wasomi ni wanasiasa tu.

Inaumiza!!

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Nadhani utakuwa umesahau kuwa awamu yake ilikuwa ni ya kuzindua na kuweka mawe ya msingi hata ambapo yaliwekwa.
FANFARE COUNTRY WHERE EVERYDAY IS A HOLIDAY.
 
Assad aliomba mikataba wa bandari ya bagamoyo uliosemwa vibaya na jabali la afrika,hakupewa,aliomba pia pafanywe uchambuzi tuone Kama bwawa la rufiji na she Zina faida,akastaafishwa
Ni zao la Msoga gang alimjua.

Si alikuwa CAG wa JK mbona hakumusaidia kuumaliza ufisadi.
 
Magufuli alisema yake , wananchi hawakuonyeshwa mkataba.

Waziri naye leo kasema yake ati hakuna mkataba uliosaniwa. Wakati video clips zinaonyesha enzi Kikwete anasaini na watu walishuhudia.

Yaani sarakasi utafikiri nchi hii wasomi ni wanasiasa tu.
Pamoja na ukichaa wote ule, lakini hakuthubutu kuonyesha mkataba watu waone kilichomo ndani. Ikabakia kusema maneno pembeni tu kama kawaida.

Waziri aliyeteuliwa na huyo kichaa, na yeye sasa anakana kuwepo kwa mkataba. Sasa bosi wake alikuwa akizungumzia masharti yaliyotoka wapi?
 
Ni profesa,kafundisha wachambia tissue pale udsm wengi tu na aliwatoa ujingani,akapewa ofisi kubwa ya taifa,akaifanya kazi vizuri tu Hadi akina yohana wakamwona kitisho
Acha lugha chafu wewe. Wanafiki tu nyinyi eti kiti moto mnaruhusiwa kula ila kama unaila tu kwa kujificha siyo hadharani.
 
Aliamini CCM ni ile ile, aliwaambia Kenya bungeni kwao pia kwamba mambo hayatabadilika hata yeye akiondoka.
 
Ni zao la Msoga gang alimjua.

Si alikuwa CAG wa JK mbona hakumusaidia kuumaliza ufisadi.
Unafiki dhambi, Assad kila mwaka alitoa ripoti ya ufisadi wa wafanyakazi hewa, ila JK alikuwa zezeta aliyeacha nchi ijiendee tu.
 
CCM imeshawazoea watanzania vibaya sana ndio maana adabu,na heshima kwa watanzania haipo.Wamezoea kufanya vibaya na hawatabadilika kamwe tutaendelea kusikia ujinga na upumbavu mwingi tu na hakutakuwa na mabadiliko yoyote kutoka CCM Kwa sababu kila mtu kwa CCM ya sasa na serikali yake ana maslahi binafsi ndio kauli mbiu yao,na UWEZO WA KUSIMAMIA SERIKALI ULISHAISHA ZAMANI SANA.NDIO MAANA HAWAJALI CHOCHOTE KUHUSIANA NA MAISHA YA WATANZANIA.Siku yaja tena kwa kasi kubwa.
 
Back
Top Bottom