Hivi kwanini mkisomesha ndio roho zinataka kuwatoka. Starehe zingine hata kama zilikuwa za gharama zaidi huwa hamlalamiki.
yes sir!
viherehere vya wanaume sometimes vinacost. Hivi unasomesha mwanamke ni mwanao? Kama umeamua kumpeleka shule kaa kimya. wazazi kuwasomeshha watoto wao wanalalamika?
Pole sana kijana, umengiea choo cha kike .
hebu rudia tena kujibu, kwa maneno mengine..
Hili jambo lipo sana...japo katika sura tofauti.
Kwamba mwanaume anaamua kumuendeleze mwenzi wake...ila mwanamke akishaendelea anaona kwamba yeye sio wa 'class' ya yule mwanamme....na hili linasababisha wanaume wengi kuwa na hofu ya kuwekeza katika maendeleo ya wanawake....
si amekutana na njemba huko chuo wamedanganyana 'i love you,i love you too' baada ya mechi kadhaa anapigwa chini hapo ndio atalijua jiji na huku kwa mwanzo kaishanyea.Huyo jamaa mpya naye anampenda huyo binti kama yule wa zamani?? Mwambie huyo kama naye anapendwa si vibaya kumwambia mapema mfadhili wake namna anavyofeel. Lakini awe makini baadae asije kulia maana huenda huyo jamaa mpya anataka kumvua tu nguo...
What goes around comes around!! Mitoto ya kike ndivyo ilivyo,sio wote msije kunimeza hapa,lakini hili huwa ni kosa sana kwa kina kaka kujifanya mnahuruma sana kwa kina dada wakiwa na matatizo,hapo utakuta mshkaji dada zake hajawasaidia hata robo,utakuta mama yake anashida sana lkn kamsaidia dem mpaka basi,usimpende mwanamke akiwa kwenye matatizo mapenzi ya kweli yaje tu sio kwenye matatizo ndio mapenzi,hizi kesi ni nyingi sana mitaani,
Kila jinsia ina matatizo, awe mwanamke au mwanaume, ukiwa na uwezo wa kumsaidia mtu au mpenzi wako msaidie, mtu aliyestaarabika na mwenye ubinaadamu hatokugeuka, na pia kama mtu anakusaidia, usimzuie kuwasaidia ndugu zake pia, ndugu zake wamempa support mpaka akafanikiwa kuwa na uwezo wa kukusaidia wewe, mkumbushe awasaidie ndugu zake pia, vilevile msaidie kumshauri afungue miradi mbalimbali ili ajiongezee kipato zaidi, kukusaidia wewe kusirudishe nyuma maendeleo yake katika maisha.
Inabidi awe makini...Asahau kuolewa. Mtu mpya atakuja kusepa in future. What goes around comes around!
mi ninavyoona ni mapenzi maana mapenz yakiisha tu hakuna jipya hapoHuyo dada akae chini na afikirie upya jinsi alivyopendwa kwa dhati na kusaidiwa na kaka wa kwanza. Ajiulize ni nini amepungukiwa yule kwa kwanza? Ni mapenzi? Au ni muonekano tu wa nje? Je, ni tamaa tu ndio inataka kumuondoa kwa mpenzi wake wa dhati? Mambo madogo madogo ya kishamba aliyoyaona yeye kama ya muonekano wa kimavazi, au utanashati yanaweza kurekebishika, ushauri wangu kwa dada, asimuumize mpenzie maana anaweza kuja kujuta maisha yake yote. Watanashati ni wengi, na watapita abaki kwa mpenzi wake. Awali ni awali, hakuna awali mbili.