ItsMi
Member
- Sep 13, 2021
- 66
- 31
Kama tujuavyo Maendeleo ya nchi yoyote duniani hutegemea kodi kutoka kwa raia wake ili kuweza kujiendesha na kujiimarisha kiuchumi, kama ambavyo pia nchi yetu imekuwa ikifanya jitihada zaidi katika sekta hii mamlaka ya mapato nchini (TRA) imejikita zaidi kuhakikisha kila raia anatimiza wajibu wake katika kuimarisha uchumi na kujiletea maendeleo ambapo bado kuna changamoto kwa baadhi ya raia kufanya njama za kukwepa kulipa kodi kwa serikali.
Lakini pia mamlaka husika imejipanga kupambana na wakwepaji kodi na kutekeleza swala zima la kuziba mianya ya ukwepaji kodi hasa ikiwalenga wamiliki wa biashara katika maeneo mbalimbali
Mamlaka ya mapato tanzania (TRA) inalojukumu la kuhakikisha kwamba kodi zinalipwa kutoka katika nyanja zote kwa mfanyakazi na mpaka raia wa kawaida
Hivyo pia inatakiwa itoe elimu ya umuhimu wa kulipa kodi kwa serikali ambapo wananchi wakijua na kuelimishwa itasaidia kukusanya kiwango kikubwa cha kodi na kurahisisha zoezi zima la ukusanyaji kodi
Tukiangalia Katika umuhimu wa kulipa kodi moja kwa moja tunakuwa tunagusia maendeleo ya nchi kwa ujumla kwa sababu kodi hii itasaidie katika kujenga shule, Vituo vya afya, barabara na kuendeleza miradi mbalimbali yenye kuleta maendeleo na yenye tija kwa taifa letu
Hivyo tuungane kudhibiti wakwepaji kodi ili kwamba tuweze kuyafikia maendeleo
Kwa pamoja tutaweza kulijenga taifa jipya
Asante
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Upvote
0