Kulipia huduma ya Choo sehemu za umma (sokoni na stendi)

Kulipia huduma ya Choo sehemu za umma (sokoni na stendi)

MK2017

New Member
Joined
Dec 27, 2021
Posts
3
Reaction score
5
Habrini wana JF,

Mimi leo langu ni swala zima la watu (haswa sisi watanzania) kulipia huduma ya kujisaidia sehemu mbalimbali kama stendi na sikoni. Najuwa baadhi yeta tunaweza sema oooh kunahitajika usafi, sawa, mbona kwenye viwanja vya ndege kuna vyoo na vipo safi muda wote? Pia hata nchi za wenzetu (mfano New Zealand, hawalipii Public toilets).

kwa kufanya hivyo inaweza saidia jamii yetu kuondokana siyo tu na usumbufu pia magonjwa kama ya figo na matumbo, achilia mbali kudhalilika (kujikojolea au kujinyea mbele ya kadamnasi). Mfano: hapa nchini wengi wanaosafiri kwa masafa marefu bado ni wale wanaokwenda kwenye shida mbalimbali kama ugonjwa/matibabu na msiba. Pia na waonea huruma sana wazee na watoto na wenye shida za kibofu ambao hawawezi kuhifadhi mkojo kwa muda mrefu.

Tunaweza kujifunza kutoka kwenye viwanja vya ndege ambako huduma ya choo inatolewa bila gharama ya ziada kwa maana ya kuwa kila ndege inayotua kiwanjani wateja wanalipia huduma zote. Achilia mbali huko, kwa sasa kila tunaponunua umeme tunalipa na kodi kadhaa za serikali, achilia mbali ununuzi wa mafuta kwaajili ya vyombo vyetu vya usafiri.

Pia kwa maeneo ya masoko: Mfano kama soko lina vizimba 200, tukisema kila muuzaji alipie 100 kwa siku tunakuwa na 20000, kwa mwezi ni kama 600000. Je hatujapata pesa ya kumlipa mfanya usafi na kununua mahitaji ambata kwa vyoo vilivyopo hapo? Uzuri ni kuwa kwa maeneo ya sokoni watumiaji wengi ni wauzaji maana wanunuzi wengi hawakai muda mrefu hapo kupelekea kuhitaji kwenda haja (achilia mbali wale wenye dharura). Hivyo, kwa kufanya hivyo itarahisisha sana kwa wale wauzaji. Badala ya ilivyo sasa ukitaka kwenda kujisaidia kuna baadhi ya sehemu fungua ameshika mtu mmoja (siku asipokuwepo chamoto mtakiona).

Tafadhali tuanze walau sehemu chache kwaajili ya kujifunza namna ya uendeshaji na kufanya tathmini, maana kujifunza siyo dhambi.

NAWASILISHA​
 
Kaka ustufananishe na inchi za wenzetu tafadhali sisi tuna usitaarabu wetu tofaut kabisa ivo ivo vinavyosimamiwa na kulipiwa una vikutaga kwenye hali gan je visipolipiwa!??
 
Huku Marekani kunya mara 1 ni sh 20,000 nyie mnataka mtushushie mizigo yenu bure!!
 
Tatizo ustaarabu F,
Hata ishu ya usafi wa mazingira mwanzo nilidhani serikali ina uzembe kwenye kuweka dustbins kila pahala ila nikaja kujua pia waTz sio wastaarabu kabisa, wanapenda uchafu.

Mtu anakunywa mo extra, akimaliza kopo atalitupa popote atapomalizia. Lile kopo lina uzito gani hadi ashindwe kulibeba na kutupa sehemu yenye dustbin mfuko wa uchafu??

Maduka mengi yana mifuko ya uchafu nje lakini huwa haijai badala yake uchafu unazagaa tu nje.

Ukiweka choo cha bure tegemea uharibu na washenzi kukitumia kama guest.
 
Back
Top Bottom