KERO Kulipisha pesa ya taka na ulinzi kwa kila kaya kwenye nyumba yenye wapangaji wengi si sawa

KERO Kulipisha pesa ya taka na ulinzi kwa kila kaya kwenye nyumba yenye wapangaji wengi si sawa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hawa watu wanakusanya kila nyumba Elfu 2000/= kwa taka na Ulinzi lakini cha ajabu wakifika nyumba yenye wapangaji wanakusanya kila chumba 2,000/= swali langu kwa mamlaka husika je inakuwa ni haki hata kwa famili yenye vyumba hata kumi wao wanatoa kiasi kidogo.

Je, ushuru ni kwa chumba au kwa nyumba?

Naomba kufahamu hili.
 
Mkishakuwa wengi lazima gharama ziongezeke, uchafu mnaozalisha kwa kila chumba ni mwingi labda kuliko mwenye nyumba stand alone.
 
Unaelewa maana ya kaya?lipeni ada za taka acheni ubishi,yani wapangaji 12 walipe sawa na familia ya mtu moja.
 
Vipi aliye ghorofani alipe 15,000 na nyumba ya chini 3,000?
Au store ya duka 30,000 na hazalishi taka.
 
Hivo vyumba si vina wakazi?Kwa maana wapangaji?
Wanazazalisha taka.lazima walipe
Ukubwa ama udogo wa makazi hauwezi kudertermine kiwango Cha taka kinacchozalishwa na wahusika.
Wakisema wawapangie italeta mgogoro katika ulipaji
Wote mtalipa sawa
 
Hawa watu wanakusanya kila nyumba Elfu 2000/= kwa taka na Ulinzi lakini cha ajabu wakifika nyumba yenye wapangaji wanakusanya kila chumba 2,000/= swali langu kwa mamlaka husika je inakuwa ni haki hata kwa famili yenye vyumba hata kumi wao wanatoa kiasi kidogo.

Je, ushuru ni kwa chumba au kwa nyumba?

Naomba kufahamu hili.
Wako sahihi kuwatoza kila kaya maana tafsiri ya kaya inasema mpangaji ni kaya hivyo anapaswa kulipa. Pia bado nyie mnalipa kidogo sisi Dodoma kila kaya/mpangaji analipa 5,000/.
 
Back
Top Bottom