Kumbe biashara ngumu sana

Halafu unakuta inakuja mijitu na makodi ya ajabu ajabu ikiwa ugumu na machungu unayoyapitia ni Mungu pekee anayekuona.
 
Nilifungua banda la chips mambo yakawa hivi:
Nikawaajili madogo wawili wakawa wanasimamia,
Siku ya kwanza madogo wakaniambia wameuza elf 48 na viazi vimeisha, kwa kifupi biashara ilikuwa poa
Siku ya pili madogo wakanikabidhi elf sitin na kitu (achilia mbali ganji zao na zile ndogo ndogo walizokuwa wananipiga)...nikajua mambo ni mazuri...
Bwanaweee..!!!!
Mauzo yakaanza kupungua,
Mara wameuza elfu 20,
Mara wameuza elf kumi na kitu
Mara chips na mishikaki vimelala
Mara mauzo hayafiki hata elf kumi...nikiwauliza vijana kulioni ,wananiambia hata wao hawajui
Siku ya siku dogo mmoja ambaye ndo kama alikuwa incharge pale..akaniambia ameenda kwa mtaalam ameambiwa banda limepigwa giza..na jamaa mmoja hivi ambaye nae alikuwa na banda lake la chips karibu yetu...nikachoka kabisa
Dogo akaniambia inabidi nasisi
tukawange ila mambo yaende vizuri...sababu sikutilia maanani biashara ika-collapse kabisa..

Nikafungua saloni ya kiume...mambo yakawa yale yale naishia tu kulipa kodi ya chumba (maana nilikuwa napewa elf 28 kwa wiki..ambapo per day ni elf 4)..salon ipo mpaka sasa lakini kiujumla mambo ni magumu...

Nikafungua na kijiwe cha kuchoma vyuma (welding workshop) nako naona hali ni tete
Lakini nikiwauliza wadau..wanasema hizi
ngoma bila kupuliza ni mziki
Biashara ukiiendea kichwakichwa unapoteza time and resources at the same time.
 
Kwa kweli nilishafungua duka kkoo, majirani wa kaniambia nikapulize ila imani yangu haniruhusu na sinto kaa kufanya hayo mambo... Biashara haiku last mwaka nilifunga nikawa acha wapulizaji huko..
Nakumbuka kwenye ile eneo letu la maduka nilisikia kuna mmama mwenye duka hapo alikua anakuwa wakwanza kufika anafagia eneo lote mwenyewe hata pasipo muhusu anakusanya mchanga, sijui anaupeleka wapi
Hivi biashara hayo mambo ya kiganga ndo misingi yake ama?
 
Yani business bila ndumba ni kazi yani hautoboi
 
Mkuu hizo biashara zote ulizofungua ulikua unasimamia mwenyewe au ulikua zote unaweka watu?
 
60% naamini biashara bila ya ndumba huwezi kutoboa na kama huwezi ndumba basi uwe na imani Kali kweli kweli bila kuyumba!
Yani hata kwenye maisha huwez kuwa katikati, it's either uwe na dini sana au uwe wa ndumba... Katikati huwez kufanikiwa utaishi maisha ya katikati ya kuunga unga tu....huwez kuwa kama Bakhresa/mengi/makonda etc.
Hata biblia inakataza wale wavuvugu sio wa moto sio wabaridi...
 
Nimeifuatilia hii thread nimeona kabisa ni halali kwa baadhi ya watu biashaza zao kufa...mtu anaulizwa ulikuwa unafanya biashara gani hataki hata kuitaja...hawajui humu kuna watu wana experience wanaweza kukwambia labda bwana umefanya makosa kwenye eneo hili na hili
 
Huyu itakuwa alikuw Anauza mahitaji ya nyumban maana hii biashara inahitaji experience ya hali ya juu kwenye biashara hii usipochangamka unawez Ukajikuta unapekechua mpaka mtaji unakula
 

Ndio nilichokuwa nasema mm hapo juu. Hizi mambo zipo bana. Mimi mpaka nafunguka hapa ni kwamba nimeyaona. Hahaha

Jamani mwenye upendo wa dhati anifungukie fundi wa uhakika inbox. Ahsante

Acha nionekane sio ila mm napigania haki na maslahi yangu Joh. Unafki Sipendi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…