Elections 2010 Kumbe EPA iliombwa na KIKWETE and LOWASSA!

Elections 2010 Kumbe EPA iliombwa na KIKWETE and LOWASSA!

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2010
Posts
7,264
Reaction score
678
Marando afyatua kombora Jangwani

Alipotakiwa kufafanua walikiukaje maadili hayo Mhando alisema: "Walikuwa hawazungumzi sera bali walikuwa wanatukana. Kama ulikuwa unafuatilia matangazo yetu utajua ni namna gani walivyokuwa wakitukana".

Hata hivyo, Mhando alisema baada ya kuwasiliana nao na kuwakumbusha juu ya makubaliano hayo walirejesha matangazo hayo hewani. Katika hotuba yake alisema kumfunga Amatus Liyumba pekee yake siyo dawa ya kumaliza ufisadi nchini, bali viongozi hao ndiyo wanaotakiwa kufungwa.

Alisema wamemfunga Liyumba ili waonekane kwa wananchi kwamba wanapiga vita ufisadi. "Jamani hivi fedha zote zilizoliwa pale Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ni Liyumba pekee yake aliyeziiba? Tunajua ametolewa kama mbuzi wa kafara," alisema Marando.

Source: Mwananchi and Marando Jangwani

Marando

"Tunajua Kikwete na edward Lowasa waliomba hela za uchaguzi kutoka kwa Mkapa akachote BOT"


My Take:

Hii Nchi inaliwa bila ya sisi kujua
Mtu anakaa madarakani kumbe ni mwizi? Kweli bado watanzania bado akili lala
 
hehehe hehehe hehe
halafu kusema na kusimamia ukweli watasema unatukana.

Endeleeni kuwachagua majizi na mafisadi mpaka watakapoanza kuguguna mifupa yenu ndo mtastuka
 
Mtei alimweleza JK kuwa uchumi hauendeshwi unavyotakiwa na mtu binafsi ila inabidi tubinafsishe mali za uma. Sera alizofanya Mkapa ni za Mtei za ubinafsishaji. Kwa mfano, alimweleza umeanzisha Azimio la Musoma la 'kilimo ni siasa' wakati limeshakufa huku ukiwataka wanachi wangojee mvua badala ya kumwagilia na miundo mbinu ya kisasa?. wakuu niko read to be corrected.
 
What a shame:glasses-nerdy::glasses-nerdy:!

Dawa ya matusi si kukatiza matangazo, dawa ilikuwa kuyasikia kwa makini ili kujenga hoja ya kumshitaki!

Wameshaona kwamba jamaa hawamwezi mahakamani, hivyo wakatumia hodhi yao ya hatamu!

What a nonsense!

These guys are in for it this term!..Hata kama Chadema haitashinda, wananchi kwa kiasi cha juu watakuwa wameelimika mno, ready for 2015!

Hoooray!
 
wale ni wapuuzi sana
kwani alikuwa anawatukana tbc?
kuambiwa ukweli ni matusi?

wa wapi hawa tbc?
 
This is reality man.
You Tanzanian,wakeup,standup and start defend your right.
Freedom for all Tanzanian.
Tunasubiri yatakuja mengi tuu na haya ni machache sana.

These guys are in for it this term!..Hata kama Chadema haitashinda, wananchi kwa kiasi cha juu watakuwa wameelimika mno, ready for 2015!

Hoooray!
 
hivi mtu mwizi ana jina lingine la kumwita mbali na hilo.....haya majitu ya CCM ni MAJIZI...
 
Nimefurahia ujasiri wa Marando na mungu aendelee kumtia nguvu kwenye kusema ukweli na fitina kwake ziendelee kuwa mwiko kwake,sasa watanzania wamefahamu kwanini JK amekuwa akimlilia Lowasa tangu alipoachishwa kwa aibu uwaziri mkuu kwa kashfa ya richmond,kumbe wote wanaunganishwa na kashfa ya epa,watanzania 2010 tuseme hatudanganyiki
 
CCM na viongozi wake wote wameoza, mwaka huu watajuta kuingia madarakani. Ninawasubiri watie mguu mitaa hii.
 
Mtei alimweleza JK kuwa uchumi hauendeshwi unavyotakiwa na mtu binafsi ila inabidi tubinafsishe mali za uma. Sera alizofanya Mkapa ni za Mtei za ubinafsishaji. Kwa mfano, alimweleza umeanzisha Azimio la Musoma la 'kilimo ni siasa' wakati limeshakufa huku ukiwataka wanachi wangojee mvua badala ya kumwagilia na miundo mbinu ya kisasa?. wakuu niko read to be corrected.

Unatakiwa uwe mkweli ama usiseme kitu ambacho huna uhakika nacho.

Makosa: Siasa ni Kilimo, siyo Azimio la Musoma, hilo ni Azimio la Iringa mwaka 1972. Azimio la Musoma lilikuwa ni UPE mwaka 1977.

Siasa ni Kilimo au kama wewe ulivyoiita, Kilimo ni Siasa, vina uhusiano gani na Mtei ambaye alikuwa ni Gavana wa BoT au Waziri wa Fedha wakati akiwa anafanya kazi serikalini?

Kuna nchi nyingi sana zimefanya economic reforms, lakini hazikufanya kwa holela kama tulivyofanya sisi. Reforms tulizozifanya zilifanyika kwa kukurupuka bila ya maandalizi. Yaani mnabinafsisha kwanza ndipo mnakuja kutunga regulatory authorities na sheria zake, mfano akina SUMATRA na EWURA wamekuja baada ya kukamilika zoezi la kubinafsisha, vitu ambavyo vilitakiwa viwe vya kwanza kufanyika kabla ya zoezi lenyewe.

Kwa hiyo hata kama Mzee Mtei alikuwa pro-economic reforms huwezi kulinganisha na madudu ambayo yamefanywa serikali ya CCM tangu tulipoanza kufanya hizo reforms. Kila tulichouza/kubinafsisha tuliishia kuliwa hakuna ambacho tulibinafsisha kwa faida. Kuanzia NBC, ATCL, TANESCO (kaburu wamekula wakaondoka), TTCL (wajanja wamekula na sasa tunatoa macho), TRC ndo hiyo imeenda na maji, wahindi wamelamba na wameishia zao, akina BANDARI shughuli tumekabidhi kwa kina Karamagi (TICTS). Hakuna ambapo tulifanya kitu kwa usahihi, kila kona ni kuliwa tu.
 
nitaweka video hiyo hapa ili watu waone kama ni matusi
 
Wewe peke yako ndio hujui haya yamesemwa sana kwenye viombo vya habari.

Mkuu hapo hujanielewa kuliwa nchi Najua vyombo vya habari vinapiga kelele kila siku lakini hakuna linalofanyika
Nchi kuliwa bila ya kujua maana yake wananchi wako usingizini "nguvu ya umma" ndo inabidi iwashughulikie hapo ndo
watakuwa wajua
 
Duh sasa naweza kutegua kitendawili kilichonishinda kukitegua kwa muda mrefu.Uswahiba wa Kikwete na Lowassa ni EPA.
 
Nyambafuuuu tbc1..........................tunasubiri nini kumkamata kikwete na lowasa na kuwawajibisha?????????????
Kweli kuna watznzania nchi hii...au wote sio raia yaani ni wahamiajai kwa hiyo tuna uraia wa kuomba sio wa kuzaliwa........
 
Nakumbuka nilishawai kusema kuwa Kesi za EPA ni danganya toto hakuna litakalofanyika hao waliotolewa kafara watapeleka mahakamani kila siku tarehe inasogezwa mbele mbisho uchaguzi ukiisha utasikia hawana kesi ya kujibu hivyo kesi imekwisha. Ikiwa Mramba anakesi mahakamani lakini amepitishwa kugombea ubunge kwa chama chake unafikiria kuna jipya hapo.... hakuna halafu utasikia kwenye kampeni Mzee wa Uzinduzi atakwambia yuko makini wale wote walio na tuhuma za EPA na nyinginezo nimewafikisha mahkamani sheria ifuate mkondo wake kha! :mad2:
 
Inauma sana!
Inauma sana!
Inauma sana!
Inauma sana!
Inauma sana!
Inauma sana!
Inauma sana!
jamani cha kufanya ni kuandika hii sms na kuisambaza kwenye simu haraka iezekanavyo.
 
Yaya- Yaani wamechunguza mamemaliz na kama yangekuwepo lazima wangeanikaa hadaharani
 
Back
Top Bottom