Kumbe gari la Wema Sepetu kimeo

Kumbe gari la Wema Sepetu kimeo

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Kumbe lile gari la kifahari aina ya BMW ambalo muigizaji nyota wa filamu Wema Isaac Sepetu ‘Madam' alizawadiwa wakati wa bethidei yake na kuwa miongoni mwa sababu za kumwagana na mpenzi wake wa awali, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz' mwaka jana, linadaiwa kuwa kimeo kwa vile limekuwa likiharibika mara kwa mara, Amani lina stori kamili.

Mapema wiki hii, paparazi wetu alikuta gari hilo likiwa limebuma mitaa ya Victoria, Kijitonyama jijini Dar es Salaam huku mshindi huyo wa Shindano la Miss Tanzania mwaka 2006 akiwa ndani, lakini ili kukwepa aibu, aligoma kutoka nje kuomba msaada, badala yake akabakia ndani huku akijaribu kuwasiliana na watu wake wa karibu.

Mmoja wa wasaidizi wake wa karibu, Petit Man baadaye akitumia gari jingine alifika eneo hilo akiwa ameambatana na fundi, ambao walilisukuma hadi eneo salama na kuliegesha. Wema alibakia ndani ya gari hilo wakati fundi akijaribu kurekebisha dosari ambayo haikuweza kufahamika mara moja.

Hadi gazeti hili linaondoka eneo hilo baada ya juhudi za kumpata ili azungumze kugonga mwamba, hakukuwa na dalili za kupatikana kwa ufumbuzi.Mtu wa karibu na Madam aliliambia gazeti hili kuwa gari hilo limekuwa likimsumbua kwa muda mrefu kiasi kwamba wakati mwingine hulikumbuka gari aina ya Nissan Murano, ambalo alipewa na Diamond siku hiyohiyo ya bethidei yake, lakini akaliuza baada ya wawili hao kutofautiana.

Baadaye Wema alitafutwa kupitia simu yake ya mkononi, lakini haikuweza kupatikana ili azungumzie juu ya gari hilo, ingawa siku za nyuma wakati gari hilo lilipokutwa likiwa limetolewa matairi eneo la Komakoma, alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa anahisi BMW hilo lilikuwa limetumika sana kabla ya kupewa kwa vile limekuwa likimsumbua mara kwa mara.

GPL
 
Attachments

  • 1434013114227.jpg
    1434013114227.jpg
    55.4 KB · Views: 894
Mama ubaya na wewe utang'ang'aniaje magar ya kifahari wakat kuyatunza huwezi? Yani mnapenda mambo makubwa pesa hamna mxiuuu, ona sasa unavyoaibika, si uliuze ununue vits tu? Mbona jokate anaendeshaga carina na yuko poa? Tatizo unapenda kujifanya una hela wakat ushuzi mxiuu na ngoja siku likuwakie moto ndo ukome, hayo magar ya kifahari waachieni akina LADY JAYDEE wenye pesa zao ooh shaur yako
 
Kumbe wanaume nao huwa wanatoa msonyo😉
 
Magazeti nayo, kwan gari kuzima ni kitu cha ajabu?

Ndio maajabu, mtu anayemilik duka south na kununua nyumba ya million 400 then gari limzimikie kila siku ni aibu sana ,kama hawez kulitunza auze anatuwekea folen za ajabu ajabu barabaran
 
SI anajifanyaga ana hela sana ,mbona atengenez gar lake, kila siku linamuaribikia yeye tu mxiuuu auze kama hana uwezo wa kulitunza

duuuhhh...!!!binamu na wema..
eti umeskia habar ya saleh bamdogo daimond
 
Ndio maajabu, mtu anayemilik duka south na kununua nyumba ya million 400 then gari limzimikie kila siku ni aibu sana ,kama hawez kulitunza auze anatuwekea folen za ajabu ajabu barabaran

Binamu na wema ninavyokujua tutabishana hadi kesho ngoja tu nikuache, ila kuharibikiwa sio ajabu bana
 
Ndio maajabu, mtu anayemilik duka south na kununua nyumba ya million 400 then gari limzimikie kila siku ni aibu sana ,kama hawez kulitunza auze anatuwekea folen za ajabu ajabu barabaran

Kwa mtu kumiliki jumba la kifahari la milioni 400 means account yake angalau ina 1bilioni so gari likizingua unapiga mnada unanunua jipyaaa!
 
Back
Top Bottom