Kumbe hata wana CCM wanalalamika?

Mwanamume

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
271
Reaction score
216
Nimepitia dukuduku na maoni katika kurasa tofauti tofauti za mitandao ya kijamii nimeona watanzania wote wanaongea lugha moja. Sioni tofauti kati ya wana CCM na wapinzani, wote wanalalamika.

Wote wanalalamika kuhusu
  • Tozo za miamala
  • Bei za mafuta
  • Maisha magumu
  • Hamza kuitwa gaidi
My take: Wana CCM tuweke ushabiki wa vyama pembeni hasa wakati masuala ya muhimu yanapo bishaniwa. Mwisho wa siku sote tunaumia.
 
Kwa hio ule usemi wa ya nini kugombania fito wakati nyumba tunayoijenga ni yetu unachukua nafasi yake
Au sio!?
 
Kewani wana CCM siyo binadamu? Acheni roho mbaya. Kama wana CCM ni wanadamu basi lazima wapo watakaolalamika na watakaonyamaza hata kama wanaumia au kufaidi inategemea mtu yuko kundi gani.
 
Kewani wana CCM siyo binadamu? Acheni roho mbaya. Kama wana CCM ni wanadamu basi lazima wapo watakaolalamika na watakaonyamaza hata kama wanaumia au kufaidi inategemea mtu yuko kundi gani.
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Si kweli

WanaCCM wangapi?

Tawini kwetu wote wanaunga mkono TOZO hii na wameshukuru kutoondolewa

Binafsi ninaiunga mkono kwa kuwa imekwenda KUJENGA VITUO VYA AFYA VINGI MNO

#TozoNiMuhimu
 
Huku kwetu ukimuonyesha mtu wa tigopesa kadi ya CCM hakukati tozo, hata petroli ukimpa attendant kadi ya CCM halafu akai scan Bei ya mafuta inashuka.

Hata wanawake wa huku ukimuonyesha kadi ya CCM hakuombi yakutolea Wala nauli hakuombi.

Ndio maana huku tunasema kazi ya kupandishwa Bei kila kitu iendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…