Kumbe HIV ni silaha ya kibayolojia iliyotengenezwa Marekani!


Mkuu,haya mambo bado yanabaki kuwa ni rumors kwani hata science haijathibitisha hivyo kwa 100% na kinachofanyika sasa ni kuzitengeneza hizo 'conspiracy theories' ili kuzivuruga akili za watu.
Nashindwa kumuelewa huyo mtaalam anaposema 'the HIV enzyme seeks out a receptor site in the blood of the Black genome. The receptor site is the CCR5 Delta 32+ (positive) gene that all people of color have'

Nijuavyo mimi ni kwamba;virusi vinavyosababisha UKIMWI(HIV-virus),ili viweze kuingia na kuziharibu chembechembe hai za kinga ya mwili wa binadamu(white blood cells aina ya CD4+ T lymphocytes) ni lazima zipate 'vipokezi'(receptors) vya kuruhusu virusi hivyo viingie ndani ya chembechembe hizo.
Hivyo vipokezi(receptors),kwa kitaalam ndiyo vinaitwa CCR-5(chemokine Receptor-5) ambavyo ni normal part of the cell.Sasa hizi receptors zenyewe ni proteins in nature na utengenezwaji wake uko genetically controlled.Sasa kukitokea 'makosa' katika utengenezwaji wake(mutation of the gene responsible for CCR-5 synthesis),ndiyo kunatokea vitu kama alivyosema huyo mtaalam hapo juu,yaani Human gene mutation CCR-5 delta 32.Sasa hii mutant gene CCR5-delta 32 haina muundo sawa na kazi sawa na ile normal HIV virus receptor CCR5,kwahiyo inamfanya mtu ambaye anazo asiambukizwe virusi vya Ukimwi kwakuwa hizi mutant receptors haziruhusu virusi kuingia kwenye kinga ya mwili na kuiharibu.Sasa basi;Inasemekana kuwa karibu 15% ya wazungu wana hizo mutant receptors yaani CCR5 delta 32 au unaweza kuwaita CCR5 delta 32+ na sisi weusi na waasia hatuna hiyo kitu yaani ni CCR5 delta 32-.Kwanini hawa wazungu wana hizo mutant gene?Wataalam wanaamini katika
historia.Kwenye karne ya 13 kulikuwa na outbreak ya bubonic plaque katika bara la ulaya.Iliwaua sana,lakini faida zake ikaleta hiyo mutation na vizazi vyao vikarithi na hivyo kuwafanya leo hii wawe resistant to HIV virus.Ukiweza unaweza ku google 'Black disease' na watakupa maelezo ya kutosha kuhusu hiyo historia.
Lakini pia watafiti wanasema kuwa virusi vya UKIMWI havitegemei njia moja(CCR5 receptor) ili kuingia katika cell za kinga za binadamu.Wamegundua pia kuna receptors nyingine zinaitwa kitaalam CXCR4 ambazo pia zinaweza kutumika kama njia ya HIV Virus.Hapa ndipo hii theory ya kusema wazungu wana kinga ya maambukizi kwa sababu wana CCR5-delta 32,inakuwa haijitoshelezi kwasababu wazungu nao wanaweza kupata maambukizi kwa hii njia nyingine kama wana kinga na ile njia ya kwanza.

Mkuu,ndiyo mana nimeanza kwa kusema hizi bado ni rumors.Kuna sheria moja ilipitishwa Marekani mwaka 1971 wakati wa Nixon,inaitwa public law 91-171 ndiyo hiyo wanaharakati hasa waamerika weusi wanataka a full disclosure ili waujue ukweli.
Baadhi ya mambo yanayosemekana kuwemo ndiyo hayo kama anavyodai huyo mtaalam kwamba ilipitishwa hiyo sheria ili kitengenezwe kijidudu cha kuwaangamiza watu weusi;synthetic disease causing microorganism that could differ from any other disease causing organism and for which no natural immunity could have been acquired and that synthetic agent could become a killer of mass populations.
Kwa mengi zaidi unaweza ku google pia hiyo public law 91-171.
Labda Obama akija kuwa Rais basi aweke wazi hiyo public law ili kukata mzizi wa fitina!
 
NIliambiwa kuwa Pan Africans wanaamini kuwa HIV ilitengenezwa kwenye maabara moja katika kambi ya kijeshi huko Marekani sijui zaidi

Labda hapa mtanifungua macho zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…