Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,439
- 145,410
Nini umuhimu wa kuua raia wasio na silaha?Baada ya kuuawa mzee wa miaka 80+ ambaye angeweza kujifia hata na presha,kisukari au kiharusi nini umuhimu wake ?
mlisema hapa kuwa ni rahisi kupata koromeo la shetani kuliko kumuua ayatollah, amekuwa mzee tena? na siyo mtukufu ayatoula?Baada ya kuuawa mzee wa miaka 80+ ambaye angeweza kujifia hata na presha,kisukari au kiharusi nini umuhimu wake ?
Tuwaulize Israel na Marekani wanaweza wakawa wanajua licha ya kwamba wanawataka hao hao raia wauangushe utawala na wawaunge mkono hao hao wanao wauaNini umuhimu wa kuua raia wasio na silaha?
Kwa nini unanijumuisha kwenye ujinga wa watu wengine ? Unapojadiliana nami zungumzia nachoandika sio maoni ya watu wengine.mlisema hapa kuwa ni rahisi kupata koromeo la shetani kuliko kumuua ayatollah, amekuwa mzee tena? na siyo mtukufu ayatoula?
hatuna haja na babu wa miaka 80+ anayefadhili mauaji ya wajukuu zake wasio na hatia, amepelekwa panapomstahili tena kacheleweshwa sana,Kwa nini unanijumuisha kwenye ujinga wa watu wengine ? Unapojadiliana nami zungumzia nachoandika sio maoni ya watu wengine.
Una miaka mingapi bwana mdogo ?
Israel na Marekani ndo waliowaua waandamanaji wa Iran?Tuwaulize Israel na Marekani wanaweza wakawa wanajua licha ya kwamba wanawataka hao hao raia wauangushe utawala na wawaunge mkono hao hao wanao waua
Israel na Marekani ndo waliowaua waandamanaji wa Iran?
Kila siku tunawaambia, mossad ni tawi la CIA,wanapewa intelligence mpaka gadgets
View: https://youtu.be/OGPcWKBWiz0?si=LN83QgAZlt2Zufl6
Kama nilivyokuwa nahisi, kazi ya ujasusi dhidi ya Ayatollah ilifanywa na CIA ya USA.
CIA kumbe walikuwa wanamfuatilia kwa kipindi kirefu tu ili kuijua mienendo yake.
Na ni CIA hao hao ndo waliowapenyezea IDF taarifa za kwamba Bw. Ayatollah atafanya kikao na makamanda wake hapo ofisini kwake alipoliwa kichwa.
Iran wameonyesha udhaifu wa hali ya juu sana.
Yaani hata Osama Bin Ladin kawazidi maarifa katika mambo ya kujificha maana CIA iliwachukua miaka 10 hadi kumpata na kumuua.
Na Osama alikuwa yeye na kundi lake dogo tu la Al Qaeda.
Sasa taifa kubwa hivyo kama Iran linakosaje mikakati imara ya kuhakikisha viongozi wake hawapatikani kiboya namna hiyo?
Kwenye haya mambo bana inabidi mtu uwe mbunifu katika kutengeneza mazingira ya kinadharia ya yale yanayoweza kutokea.
Mfano, yaelekea Iran walidhani kuwa mashambulizi dhidi yake hayawezi kufanywa asubuhi kwa sababu mara zote yamefanywa usiku.
Ndo hivo Ayatollah akawakusanya makamanda wake asubuhi na mapema bila kujua kumbe ndo inaenda kuwa siku yao ya mwisho.
Ayatollah na makamanda wake ni bure kabisa. Wanachokiweza ni kufuga midevu na kuvaa kanzu tu.
Wamarekani walianza mapema kabisa kujiandaa na hayo mashambulizi. Walipeleka mameli yao ya kivita huko Mashariki ya kati, walipeleka kila aina ya mazagazaga kwenda kukaa mkao wa kushambulia.
Lakini li Ayatollah kumbe bado likaendelea kuuweka usiku hapo hapo Tehran 🤣.
Ndiyo, CIA ni majasusi mahiri sana. Lakini pia, kuna nyakati huwa wanasaidiwa kazi yao.
Katika hili, upumbavu wa Ayatollah ndo umewasaidia kuifanya kazi yao hao CIA kuwa ni rahisi sana.
Kwani nani huwa anabisha?Kila siku tunawaambia, mossad ni tawi la CIA,wanapewa intelligence mpaka gadgets