Kumbe ilikuwa wanaumia

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Mchezo wa marudiano kati ya dar es Salam Young Africans dhidi ya Club Africain umemalizika na Yanga kufanikiwa kuingia hatua ya makundi CAF Confederation Cup kwa ushindi wa bao moja bila wakiwa ugenini.

Maneno yalikuwa mengi kabla ya mechi ya leo, wengine wakisema haiwezekani. Kiufupi hakuna aliyetarajia kilichotokea leo, hata kama walikuwepo walikuwa kwa asilimia chache sana. Hongera kwao kwa kujituma na kujitoa kwenye mechi ya leo.

Sasa tujikumbushe kidogo kauli za mashabiki wao kabla ya mechi ya leo:

KABLA YA MECHI YA LEO
~ Kwani Simba huko CAF Champions League wana mafanikio gani? Kwanza kushiriki siyo mafinikio, unatakiwa uchukue ubingwa ndiyo tutajua kweli umefanikiwa.

~ Caf Confederation Cup ni Kombe la 'loser', wanaume wote wanacheza CAF Champions League.

~ Kwani Simba ikiwa nafasi ya 11 kwenye 'rank' za vilabu bora Afrika ina faida gani? Mafinikio pekee ni kuchukua Kombe.

~ Kushiriki kila mwaka bila kuchukua kombe siyo mafanikio, sisi Yanga tukipata nafasi kama hiyo tunaenda mpaka fainali na kubeba Kombe.

~ Simba anahangaika huko kimataifa, akija kwa Mkapa sisi tunajipigia tu. Muache aendelee kuzurura sisi tunamsubiria.

BAADA YA MECHI YA LEO
~ Mashabiki wameshajiandaa wanaenda uwanja wa ndege kuwapokea, sasa sijui wanaenda kuwapokea kwa lipi wakati walisema hatua ya makundi siyo mafanikio.

~ Leo mtaani mashabiki wa Yanga walikuwa na furaha sana, walishangaria toka goli lilipoingia mpaka mpira unaisha. Sasa sijui walikuwa wanafanya hivyo kwasababu gani, wakati walisema mafanikio pekee ni kuchukua ubingwa?

~ Kupitia msemaji wao, walisema Kombe la Shirikisho ni kombe la 'loser', wakati huo Simba katolewa CAF Champions League kaenda CAF Confederation Cup mwaka jana, leo hii limekuwa UEFA Champions league?

~ Baada ya mpira kuisha wachezaji na viongozi waliingia uwanjani kushangiria mpaka Waarabu wakaanza kurusha chupa, sasa sijui walikuwa wanafurahia nini wakati ile haikuwa fainali, ilikuwa ni mechi ya kufuzu tu kwenda hatua ya makundi CAF Confederation Cup. Inashangaza sana na kufikirisha!

NB: Wananchi huu ni wakati wenu kuwaonesha njia Simba kwenye mashindano makubwa kama haya, tunawasubiria tuone mtacheza na nani fainali, maana mna wachezaji wazuri na timu bora.
 
Hakuna kiumbe chenye unafiki kama kinachokuwa na vinasaba vya utopolo.Miaka yote ndiyo hivyo.Roho zilikuwa zinawatukutia kuliko unavyoweza kudhania.Ni nani anafurahia kuitwa "mihogo-kivunde fc"?😂😂😂😂
 
Una ujinga mwingi sana rudi shule.
Sana tena kesho jiandae kwenda airport kuwapokea mashujaa wa nchi kwa mara ya kwanza toka uhuru nchi inatoa muwakilishi wa Caf champions league na kufika hatua ya makundi.
 
Maneno ya kujifariji baada ya kutokea kile ambacho hamkukitegemea..
Jiandae kwenda airport kuwapokea mashujaa wa nchi kesho wanaenda mpaka ikulu moja kwa moja wakitoka wanaenda bungeni.
 
Mnaenda kuwapokea wachezaji kwa kipi walichofanya? Kuna kombe wanakuja nalo kutoka Sudan au
Na nyinyi muende sasa mkawapokee wachezaji wenu, badala ya kubwekabweka tu hapa. Maana ilibakia kidogo tu waangakie pua.
 
Na nyinyi muende sasa mkawapokee wachezaji wenu, badala ya kubwekabweka tu hapa. Maana ilibakia kidogo tu waangakie pua.
Tulikubaliana mkuu mafanikio ni kuchukua kombe tu sasa mnataka mkawapokee kwa lipi wanakuja na kikombe gani kutoka huko Sudan maana tunajua simba na yanga hazina mafanikio yoyote Caf champions league sasa mbona nyinyi mnatuzunguka mnaenda kuwapokea wachezaji wenu tena mnawaita mashujaa.
 
Wenye Akili ni 2 tuu hapo dimbwini kumbuka
Walipiga sana kelele wakasema mafanikio ni kuchukua kikombe kufika nusu fainali au robo fainali sio mafanikio nashangaa wenzetu wanataka wakawapokee mashujaa na wanataka waende ikulu na bungeni wakapewe heshima yao [emoji1787][emoji1787] maajabu haya.
 
Cheki ili jinga halijui ata kinachoendelea Lina andika pumba,yanga wanatoka Sudan?
 
 

Attachments

  • Tablem.jpg
    78.7 KB · Views: 4
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…