Kumbe Jk Bado Mtu wa Watu!

Kikwete sio mtu wa watu ila ni mtu wa mijitu(mifisadi, mitendaji mizembe, mila rushwa,) hao ndio watu wake na yeye ni mtu wao na mtetezi wao. Hivi wanaopenda kikwete na ccm ni warz kweli?
 
mtu wa watu wapi? unafikiri kutafuta umaarufu mpaka msibani ???????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Jk hana shida isipokuwa watendaji wake ndio wanao muangusha.
 
Cheap popularity, mambo nyeti ya mstakabali wa taifa haonekani lakini mambo ya kipuuzi kama kuhani msiba ya mwana maigizo mbakaji wa under 18 anakwenda

Pole, pole, Huihui2. Lulu alifanya sherehe yake ya kutimiza miaka 18 mwaka jana, kwa hiyo marehemu sidhani kama alim-mbaka, mimi na baba 'D' tumepishana miaka kumi na mbili na wanandoa wa aina hii, wapenzi wapo wengi tu, hawa naona walikuwa wamepishana miaka kumi, na kutokana na mambo mengi ambayo tumeshawahi kusikia yakisemwa kuhusu lulu japo hatuna uhakika, sishangai hata kidogo yeye kuwa na marehemu kwani wamepishana miaka kumi. Samahanini kwa wale ambao wanaona marehemu alikuwa anam-mbaka lulu, halafu jamani tumuoneeni lulu huruma, unajua akitoka mama/baba wa marehemu, pamoja na ndugu wa karibu wa marehemu (hawa tuwaweke kundi moja), Lulu ndiye atakuwa mfiwa wa pili, maana amefiwa na mupenzi. Sijui angekuwa amekufa kifo cha kawaida angejitokeza kusema yeye ndiye mpenzi wa marehemu au wangejitokeza wengi zaidi, maana hatukusikia kabisa habari za mpenzi wa marehemu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…