johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Jana baada ya kumsikiliza kwa makini Waziri Nape pale Clouds TV ndio nikaelewa kwanini hayati Magufuli alikuwa anasema mambo yote anayofanya bunge linayajua na limeyabariki.
Nape alisema kamati za bunge ndio hufanya kazi zote za msingi na mwisho hukubaliana na kutoa maoni ya pamoja.
Kwa mfano ununuzi wa ndege kamati husika ya bunge kama ilitaarifiwa na kuafiki hapo ni bunge limeafiki hata kama Chadema wabunge wao watajifanya kupinga pinga baadae.
Kwa Tanzania ni ngumu sana serikali kujiamulia kufanya jambo lolote bila baraka za bunge na hii ni tangu enzi za mfumo wa chama kimoja.
Yaani Serikali inunue ndege zaidi ya 10 bila akina Tundu Lisu kujua na kupitisha pale bungeni? Isingewezekana kabisa bwashee.
Maendeleo hayana vyama!