Kumbe kuna walimu ni boda boda

moesy

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2012
Posts
3,555
Reaction score
3,536
Nimebaini kuna idadi ya walimu wanaofanya kazi ya kuendesha pikipiki(boda boda) ili kuingiza kipato. Ayo nimeyabaini wiki iliyopita Musoma baada ya kukodi pikipiki na kubaini dreva wangu ni mwalimu by proffesional.

Baada ya kumdadisi kwa undani akanieleza wapo si chini ya walimu 9 (primary na sekondari) wanaofanya kazi ya bodaboda, na sababu kubwa ni kipato kidogo wanachopata kwenye mishahara yao.

Na shughuli iyo imekuwa ikifanyika ata muda wanaokatakiwa kuwepo madarasani.

Je kuna mwanaJF mwenye kujua kuhusu lolote kwenye mikoa mingine?
 

Kiongozi upo sahihi kabisa, baada ya Serikali kuwawezesha mishahara yao ipitie NMB basi wakawa wanakopesheka, wengi wao walipokopa wakaingia kwenye hiyo biashara inawalipa kwa kweli ingawa upande wa pili unaathirika
 
Kweli ata mimi nilishapata bodaboda ambapo teacher alikuwa dereva...ndio nchi zetu uchumi wote upo chini ya wanasiasa
 
katika ajira isiyokuwa na heshima ni ualimu, kuanzia mshahara marupurupu na utendaji
Hakuna hata siku ukasikia bungeni kukwamisha bajeti eti mishahara ya walimu kuboreshwa
karani wa wizara yoyote ya serikali hii anaheshimika kuliko mwalimu, wakati hana hata diploma kulinganisha na mwalimu aliye graduate

Serikali ifanye katika siasa iwe ajira ya kujitolea na mishahara ya wanasiasa wapewe walimu ndio utajuwa kiwango cha elimu kitakavyokuwa hapa Tanzania
 
Maskini waalimu wamekuwa
yatima sana hii nchi,alafu mnakaa mnapiga hesabu waalimu watoe div1,2,3?
..kalagabao bwana.

kwani n dhambi huyo mwalimu kumilk Bodaboda?
 
kwani n dhambi huyo mwalimu kumilk Bodaboda?
ishu siyo kumiliki boda boda,ni kuwa dreva wa iyo boda boda kuendesha biashara ata wakati wanatakiwa kuwa madarasani kufundisha,NB rudia kusoma thread line by line utaelewa.
 
Mm pia ni shahidi wa hilo, mwaka jana nlkuwa mkoa wa mbeya, wilaya ya rungwe maeneo ya kiwira, dereva bodaboda nilyopanda ni mwl wa shule moja ya kata palekiwira, nilipobain kuwa driver ni ticha nikahoji kulikon saa 7 mchana upo hapa badala ya shulen? majibu yake yalikuwa hivi.

1: mimi ni mwl sawa lakin si muda wote natakiwa kuwepo darasani, kuna muda wawanafunz kujisomea.
2: kwa siku nina vipindi 2-3 nachofanya nafundisha asubuh kimoja au viwili na baada ya break(saa 6) nakuja kujishughulsha na bodaboda, maisha haya bila shughuli za pembeni hutoki, kila kitu bei juu laki nne haitoshi.

KWA HILI nawaunga mkono kwan ukipiga hesabu ya bidhaa za ndan kama sukari, unga,bili ya umeme, bili ya nyumba, mavazi, matibabu nk. laki nne mizinguo wanapiga na issue zingine kwa sababu serikali haina uwezo wa kuwaongeza mishara basi acheni wajiongezee wenyewe.
 

Afadhali ya hawa walimu mi naona wana a kili sana.Kuna watendaji wengi wa serikali muda wa kazi utawakuta bar au madanguro ofisini hawpatikani. Mi kwa mtizamo wangu jamii na serikali isitafute namna ya kuwabana walimu ili wafundishe bali iifanye kada ya ualimu kuwa kada ya kukimbiliwa badala ya kukimbiwa.
 
Kiongozi upo sahihi kabisa, baada ya Serikali kuwawezesha mishahara yao ipitie NMB basi wakawa wanakopesheka, wengi wao walipokopa wakaingia kwenye hiyo biashara inawalipa kwa kweli ingawa upande wa pili unaathirika
sasa hapo kuna masomo tena?
 

sahihi kabisa
 
sahihi kabisa.usiwe mwizi tu.kila kitu kimepanda bei kwa kasi kubwa
 
ishu siyo kumiliki boda boda,ni kuwa dreva wa iyo boda boda kuendesha biashara ata wakati wanatakiwa kuwa madarasani kufundisha,NB rudia kusoma thread line by line utaelewa.

muda wa darasani wawe darasani kufundisha,muda baada ya masomo waendeshe bodaboda
 
walimu ni lazima walipwe vizuri kinyume na hapo tunatengeneza mabomu kama hayo ambayo yameanza kulipuka
 
Mbona mnatufatafata walimu jamani. Fanyeni yenu elimu na ualimu tuachieni sisi na serikali tutamalizana kiutu uzima. Wamemwaga ugali sisi tunajua tufanyeje. Chezea mwl ww

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Nawapa hongera walimu kwa kipato halali ingawa wanakwenda majukumulakini pia wanafanya kipato halali cha bodaboda
Kuna wale wa maofisini wanaiba katika sehemu zao za kazi halafu hawakai kazini naeza sema wao ni double standard
Serikali haikuangalia nini source ya maendeleo wanafikiri maofisini ndio pekee yatapatikana maendeleo hawajui kuwa elimu ndio source na bila walimu hakuna elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…