Pre GE2025 Kumbe kweli chema chajiuza kibaya chajitembeza. Kampeni Miaka 2 kabla?

Pre GE2025 Kumbe kweli chema chajiuza kibaya chajitembeza. Kampeni Miaka 2 kabla?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Sasa nimeamini kuwa misemo ya wahenga ilikuwa inafanyiwa utafiti kabla ya kuidhinishwa.

Kwa nini kwa muda wa miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu 2025 kumekuwa na kampeni kubwa kumtangaza "mama" kuwa ni bora na anafaa kuendelea kupewa miaka mitano?

Kwa nini asiachwe afanye kazi yake na wakati ukifika wananchi wataamua?

Maana kwanza lazima chama chake kimteue kikimkubali kisha ataletwa huku kwetu WENYE AKILI zaidi tuamue.

Sasa tokea mwaka jana nguvu kubwa inatumika kutaka watu waamini yeye ni bora wakati wanaona ya ovyo mengi sana yanaendelea ikiwamo hali ya kiuchumi, ajira, huduma mbovu, WIZI MKUBWA wa mali za umma, akili za waTZ kudumaa kwa uchawa nk?

Au ndio tuamini kabisa kuwa CHEMA CHAJIUZA BA KIBAYA CHAJITEMBEZA?

kwanini asingoje ile miezi miwili ya kampeni baada ya chama chake kumpitisha ajinadi?
 

Attachments

  • FB_IMG_1717566984826.jpg
    FB_IMG_1717566984826.jpg
    95.5 KB · Views: 2
Back
Top Bottom