Kumbe lisemwalo lipo kweli!

Kumbe lisemwalo lipo kweli!

malang0

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2021
Posts
440
Reaction score
523
Wahenga wana msemo usemao lisemwalo lipo kama halipo laja, huwa jamii yetu wanasema jamii ya watu wanaofanya kazi za udereva haswa wa safari ndefu huwa wana tabia za uzinzi sana. Maneno haya yapo mtaani tangu siku nyingi hadi leo yanaongelewa, basi wikiendi iliyopita nilipata nafasi ya kusafiri safari ndefu toka Dar hadi Rock City,Mwanza.

Safari yetu ilikuwa nzuri na tunamshukuru Mungu tulifika salamaa ingawa ni safari ya kuchosha sana.Tuliondoka Dar saa 11.30 na mojawapo wa basi yenye umaarufu kwenye ukanda huo. Nilibahatika kukaa siti za nyuma za basi letu. Tulilipokuwa tunakaribia kuondoka tukiwa tumefunga mikanda yetu akapanda binti mdogo wa miaka kati 18 au 20 hivi, ila yeye hakupata siti ila alikalia ndoo ndogo.

Hapo ndipo kisa chetu kilipoanzia ikapidi nimuulize kulikoni anasafiri mwendo mrefu hivyo na hana siti, yule binti hakuwa na hiyana akaanza kufungua na kusema dereva wetu ndiyo kamwambia hivyo. Mmmh ikabidi nizidi kudadisi zaidi na kumuuliza maswali mengi. Kulikoni akukalishe kwenye ndoo na asikulipie siti?

Basi kabinti kakazidi kufunguka na kusema dereva wetu ni mpenzi wake na walikuwa wametoka kulala wote gesti moja nyumbani kwao Manyoni, Singida. Walifika saa sita usiku wakaenda kulala wote na amemlipa 30,000/=. Kwa mantiki hiyo huyo binti hakuja kutembea ila kufanya uzinzi na dereva wetu. Inamaana alikaa Dar masaa manne tuu na kisha anarudishwa kwao.

Duuh, kwa mukutadha huo ilinifanya nitafakari mambo mengi sana inawezekanaje dereva aliyepewa heshima ya kazi tena yenye kulinda maisha ya watu, madereva wenzake alichokabidhiwa chenye kumpa ugali yeye na familia yake anafanya upuuzi kama huu. Je hajijui hiyo ni kazi ya heshima sana na ulinzi wa maisha ya watu? Kwa nini anaendekeza ngono na kuacha maadili yake? Ndipo nilipokumbuka huwa watu wanasema madereva ni malaya sana kumbe kweli!
 
Wee nimesharudi punguzni tabia hizi
ila nimekafaid sana tuache za utani..
madreva tunapendw sana had mtaani maana tuna hela y uhakika,na tukirud tunabebea madem sato na majunia y mkaa..
mtu akiwa na dem wake afu dem akaniona ghafla anamkimbia msela!acha tufe tuu kwa changamoto ya kinga mwili
 
Miaka 18 tayari anapiga kura,
huyo dereva yuko sawa halafu tusisahau jamani mtoto ni mnyaturu
KwaniManyoni ndiyo centre ya ku-harbour wasichana kuja kufanya biashara ya ngono?
 
Imagine unapanda gari halafu siti uliyokalia kumbe jana yake usiku uzinzi ulikuwa unafanyika hapo kwenye hiyohiyo siti. Dah maisha ni fumbo.

MÊmENtO HoMO
 
Wahenga wana msemo usemao lisemwalo lipo kama halipo laja, huwa jamii yetu wanasema jamii ya watu wanaofanya kazi za udereva haswa wa safari ndefu huwa wana tabia za uzinzi sana. Maneno haya yapo mtaani tangu siku nyingi hadi leo yanaongelewa, basi wikiendi iliyopita nilipata nafasi ya kusafiri safari ndefu toka Dar hadi Rock City,Mwanza.
Nilivoona mada inahusu madereva na uzinzi,,, nikajua tu lazima kuna kamji katatajwa tu, na sijakosea!![emoji38][emoji38][emoji38][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Nilivoona mada inahusu madereva na uzinzi,,, nikajua tu lazima kuna kamji katatajwa tu, na sijakosea!![emoji38][emoji38][emoji38][emoji119][emoji119][emoji119]
Haka kamji ni maarufu kwa mambo haya nini?
 
Upuuzi??. we vipi?? Imeandikwa hivi "Enendeni mkazaane muijaze dunia" wape kasema mkaoane? sasa we unaweza kuijaza dunia kwa mkeo tu??
 
Madereva wa lori ndio kiboko wao hata hawaoni hasara kupaki gari wakaenda kushughulika.
 
Unakuta unamlaumu huyo dereva kwa kufanya hivyo lakini ukute hiyo ndo ponapona yenu.. bila hiyo kitu anaweza watumbukiza mtaroni..🤣
 
Back
Top Bottom