Nimeona mashabiki wakigawanyika katika mtazamo wao.
Kuna wale wenzangu mimi,tukiona timu inafanya vibaya au ina dalili za kufanya vibaya,tunaumia na kulalamikia vitu tunavyodhani ndiyo sababu.
Kuna wale wanaofaidika na club moja kwa moja kwa kupewa vipesa kidogo.Hawa ni watu wa Dar wanaojiita wanachama wa matawi ya Simba. Hawa wanasimama na kuwatukana mashabiki wanaolalamikia uongozi ama wachezaji ama hata mwalimu. Wengine wanawatukania hadi mama zao. Hii yote ni kujaribu kuwadhibiti wapenzi wa Simba wasilalamike hata kama wakifungwa.Kuna kiongozi aliwahi kuwaita mashabiki hawa mbumbumbu.
Ni kweli wengi wetu nj mbumbumbu kwa vile tumelipia app, tunaitika tukiitwa viwanjani,tunaisapoti timu tukijua nguvu yetu ndiyo inavutia wawekezaji pia.
Jambo baya sana hili.
Ninatabiri kuwa watu wengi kwa kufanywa hawana akili, kukatazwa kulalamika na kutoa maoni,wengi watarudi nyuma na kuachana na ushabiki ambao unawaumiza tu.
Maana ninachojua binadamu akilalamika, anakuwa ametoa nyongo na uchungu moyoni, anaanza upya.
Kwa sasa ninaona viongozi wanakosea kuwalipa watu wajitokeze kwenye media kutukana washabiki wenzao wanaolalamikia uchezaji mbovu.
Watani walisema bado hatujasema,nadhani wengi watanyamaza na kuachana na ushabiki wa timu inayoongozwa na kihuni na usajili wa janja janja.
Binafsi nililipia app mwaka mzima,ninaisapoti timu kwa njia nyingi,lakini sasa hadi watakapotuheshimu mashabiki, nitatulia nifanye mambo mengine