Kumbe mateja hugawana damu ya mwenzao?

Kumbe mateja hugawana damu ya mwenzao?

Mzalendo Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
735
Reaction score
191
Last week nilikuwa nasikiliza kipindi cha Radio One Doctor. Mada ilikuwa juu ya magonjwa ya akili. Mambo mengi yaliongelewa ila hili lilinishangaza sana.

Kwanza Mateja wakikosa dawa wanaenda kwa mwenzao mmoja ambaye amefanikiwa kupata dawa. Wanachukua bomba la sindano anawapa damu yake kupitia hilo bomba. Wale mateja wenye njaa wanajidunga hiyo sindano kugawana damu ya yule mwenzao angalau nao wapate hicho kilicho kwenye damu! Inatisha.
 
ni hatari kwa kweli mkuu maisha wanayoishi hawa watu ni hatari sana, kwa kifupi ni kwamba wanaishi dunia nyingine kabisa ya kufikilika huwezi amini. Nini cha kufanya? sijui, kwa sababu hao hao viongozi tunaowategemea ndio wanaoingiza hayo madawa kwa wingi sana. hata kuanzisha vituo vya matibabu kwa waathilika hawataki. inauma sana jamani ndugu zetu hawa wanapotea huku tukiwaaangalia na kuwashangaaa. so sad.
 
Back
Top Bottom