Kumbe Museveni hotuba Dodoma alimlenga Kyagulanyi (Bobi Wine)

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana pamoja na yetu machungu, hebu na tuyaone ya wenzetu katika zile chaguzi za ghiliba ambazo labda ni bora tu zisingekuwapo.

Bobi Wine aka Robert Kyagulanyi (mmoja wa candidates Uganda) hivi sasa yuko mikononi mwa polisi. Mizengwe na vimbwanga anavyokutana navyo mgombea huyu kipenzi cha wengi huko havina tofauti yoyote na alivyokuwa akivipitia Mh. Lissu katika kipindi cha kampeni.

Yaonesha Museveni na bwana yule ni baba mmoja mama mmoja. Bila shaka hata alipokuja Dodoma ilikuwa katika kubadilishana uzoefu zaidi. Na sasa yu anafuata nyayo tu kama alivyomsifia Moi (R.I.P) kwenye kufuata za Kenyatta.

Akihutubia Dodoma rais huyo mkongwe asiyekuwa na mpango wowote wa kustaafu, alidai katika vyama, yeye anajua CCM tu Tanzania. Akasema hii ni kwa sababu anajua (kwa maneno yake) "what they stand for" tokea kwa mwanzilishi wake Nyerere (rip).

Bila ya kueleza kama hata alifuatilia kujua vyama vingine vinasimamia nini, akaenda mbali zaidi kuwaasa hasa vijana kutofuata tu watu au vyama. Akijinasibu eti kwani yeye naye anasimamia uchumi kama ilivyo sisi na chama mboga mboga kuwa sasa tu uchumi wa kati.

Ni wazi kuwa huyu bwana jina lake litakuwa linapiga hodi pale ICC TMK (kwa wanaume) si muda mrefu kutoka sasa. Tofauti na sisi kwenye hii ya mabegi begi ya gwaji boy, huko watakufa wengi.

Kumbe bwana yule alianza kuweweseka muda hata kudhania Dodoma ni Koboko (Uganda).Kama ilivyokuwa kwa mzee baba, huyu naye kashikwa kubaya. Huenda naye karata pekee ya vishindo ni kama ile ile.

Hata hivyo pole yao kina Kyaguranyi. Yatakayowakuta katu ha yawezi kuwa tofauti. "Pori jingine, nyani wale wale." Mshindi kutangazwa, hajali idadi ya kura.

Si muda mrefu unaobakia kwao kina Kyaguranyi nao kama Prof. Lipumba watagundua kuwa, bila ya tume huru hamna haja ya kufanya uchaguzi wowote.

Yawezekana watawala wetu kwa uchungu wao wa kutuletea maendeleo, wamejipanga kusalia madarakani ikibidi hata kutangaza himaya zao za kifalme kinyemela.

Bila ya maamuzi magumu, safari bado!
 
✓[emoji769]Role model wa Vladimir Putin, Donald Trumpet [emoji448], Xijiping, na wahuni wengine[emoji769]
 
Safari hii Amstadam atakua na kesi nyingi ICC.

Amsterdam anashughulika na wateja wake.

Ila ICC panaweza kuwa na wateja wengi wasiowakilishwa na Amsterdam.

Katika hao angalau mwingine tokea Uganda haitakuwa ajabu.
 
Wanamlipa nini?

Na wewe una kesi dhidi ya jiwe unataka kuongeza nguvu?

Wengine wako kama kina Chuck Norris "they fight for those who can't fight back." Uliza Nyamongo Lissu alifanya sana hizi kuliko Chuck Norris.
 
Waganda hawapendi ujinga, wafuasi wake Kampala wameanza vurugu mtu wao aachiwe na polisi.

Madikteta huelewa lugha kinaponuka tu.

Tunapopambania na hali yetu si haba kuchekishia demo.

Lao na letu baba mmoja mama mmoja.
 
Nimeona polisi akichezea vitasa hapo ashukuru mwenzake aliyetokea ghafla na silaha.
hizi chafuzi Afrika bora zisiwepo tu
 
Mabibi na mabwana pamoja na yetu machungu, hebu na tuyaone ya wenzetu katika zile chaguzi za ghiliba ambazo labda ni bora tu zisingekuwapo.

Bobi Wine aka Robert Kyagulanyi (mmoja wa candidates Uganda) hivi sasa yuko mikononi mwa polisi. Mizengwe na vimbwanga anavyokutana navyo mgombea huyu kipenzi cha wengi huko havina tofauti yoyote na alivyokuwa akivipitia Mh. Lissu katika kipindi cha kampeni.

Yaonesha Museveni na bwana yule ni baba mmoja mama mmoja. Bila shaka hata alipokuja Dodoma ilikuwa katika kubadilishana uzoefu zaidi. Na sasa yu anafuata nyayo tu kama alivyomsifia Moi (R.I.P) kwenye kufuata za Kenyatta.

Akihutubia Dodoma rais huyo mkongwe asiyekuwa na mpango wowote wa kustaafu, alidai katika vyama, yeye anajua CCM tu Tanzania. Akasema hii ni kwa sababu anajua (kwa maneno yake) "what they stand for" tokea kwa mwanzilishi wake Nyerere (rip).

Bila ya kueleza kama hata alifuatilia kujua vyama vingine vinasimamia nini, akaenda mbali zaidi kuwaasa hasa vijana kutofuata tu watu au vyama. Akijinasibu eti kwani yeye naye anasimamia uchumi kama ilivyo sisi na chama mboga mboga kuwa sasa tu uchumi wa kati.

Ni wazi kuwa huyu bwana jina lake litakuwa linapiga hodi pale ICC TMK (kwa wanaume) si muda mrefu kutoka sasa. Tofauti na sisi kwenye hii ya mabegi begi ya gwaji boy, huko watakufa wengi.

Kumbe bwana yule alianza kuweweseka muda hata kudhania Dodoma ni Koboko (Uganda).Kama ilivyokuwa kwa mzee baba, huyu naye kashikwa kubaya. Huenda naye karata pekee ya vishindo ni kama ile ile.

Hata hivyo pole yao kina Kyaguranyi. Yatakayowakuta katu ha yawezi kuwa tofauti. "Pori jingine, nyani wale wale." Mshindi kutangazwa, hajali idadi ya kura.

Si muda mrefu unaobakia kwao kina Kyaguranyi nao kama Prof. Lipumba watagundua kuwa, bila ya tume huru hamna haja ya kufanya uchaguzi wowote.

Yawezekana watawala wetu kwa uchungu wao wa kutuletea maendeleo, wamejipanga kusalia madarakani ikibidi hata kutangaza himaya zao za kifalme kinyemela.

Bila ya maamuzi magumu, safari bado!
Mmebaki kujifariji. Tundu alifanyiwa kitu gani kibaya wakati wa kampeni na baada ya Oktoba 28 zaidi ya wananchi kumtia adabu na kumuonyesha njia ya Ubeligiji.
Wajumbe sio watu wa kubeza.

Wenzako wameimarisha CHAMA ngazi ya nyumba 10, wewe hata baadhi ya Wilaya huna uongozi unadai umeshinda. Siwendawazimu huu
 
Kama ni kujifariji wewe inakuwasha nini jombi?

Au ni pilipili unazozila ndizo zinazokuwasha?
 
Back
Top Bottom