Beesmom
JF-Expert Member
- May 30, 2016
- 17,202
- 28,732
Bado tupo kwenye kitabu Cha MWANZO...Bado tupo na ukoo wa Yuda....Bado tupo na mjane Tamari.
Ni kitabu Cha MWANZO 38:11-26
Baada ya mzaliwa wa pili wa Yuda kufa(Onan) ...Yuda akamwambia Tamari mkwewe,ukae mjane nyumbani mwa baba Yako hata shela Mwanangu(mzaliwa wa tatu wa Yuda) atakapokuwa mtu mzima,bas Tamari akaenda akakaa nyumbani Kwa babaye .
Siku nyingi zikapita,akafa Binti shua mkewe na Yuda.Yuda baada ya kufarijika,akaenda Kwa Watu wake wawakatao kondoo manyoya huko Timna.Huyo Tamari akapewa habari kuwa mkwewe yupo Timna,bas akavua nguo zake za ujane akajivika utaji na kujifunika USO akakaa mlangoni pa Enaimu,Karibu na njia ya kuendea Timna.
Yuda alipomwona alimdhania ni kahaba,maana amejifunika USO.Akamgeukia Kando ya njia,akasema niruhusu niingie kwako,maana hakujua kuwa ni mkwewe.Tamari akamwuuliza,Utanipa nn ukiingia?,akamjibu nitakupa mwanambuzi wa kundini.Naye akamwuliza,je,Utanipa rehani hata utakapomleta? Akauliza nikupe rehani gani? Akamjibu,peteyako ya muhuri,kamba yake na fimbo Yako iliyo mkononi mwako.Basi akampa,akaingia Kwake akampa mimba.
Basi Tamari akandoka,akavua utaji wake akavaa mavazi ya ujane wake.Ikawa baada ya miez I mitatu Yuda akapewa habari kwamba mkweo,Tamari amefanya uzinifu,naye ana mimba ya haramu.Yuda akasema mtoeni akateketezwe.Alipotolewa,alipeleka watu Kwa mkwewe,alisema "Mimi nimepewa mimba na mtu mwenye vitu Hivi,akasema ,Tambua basi vitu hivi ni vya nani,Pete hii.Yuda akavikiri,akasema yeye ni mwenye haki kuliko Mimi,Kwa kuwa sikumpa Shela Mwanangu(mzaliwa wa Yuda wa tatu kama alivyoahidi)
Kumbuka Eva(Hawa) Kwa Adam,mke wa boss Kwa Yusuph,....japo Tamari kazidisha kipimo....Muwe na jumapili njema wanajf.