Kumbe ni kweli ulimi wako unaweza kuwa laana kwako ukiutumia vibaya

andazi

Member
Joined
Jun 7, 2025
Posts
63
Reaction score
269
Kumbe kinachosema watu kuwa ulimi wako unaweza kuwa laana kwako ni kweli. Kuna dada mmoja hapo nyuma aliachana na mume wake baada ya kufungua kibiashara chake ambacho kilikuwa kinamuingizia pesa.

Dada uyo alimchafua mume wake kwa kumtukana mpaka kwenye mitandao ya kijamii TikTok uko akishauria wanawake wenzake kuwa mwanamke anaweza bila mwanaume wasijitese kwa ndoa ambazo haziwapi faida yeyote zaidi ya manyanyaso.

Alishauriwa na watu wazima mpaka na vijana wenzeke kuhusu tabia iyo ya kumchafua aliyekuwa mume wake mitandaoni aliona wanao mshauria ni vichaa tu.

Maisha yaliendelea kwake kama kawaida akaanza kuona mabadiliko kidogo kidogo kwenye biashara yake kumbe wateja wake wengi walikuwa wameolewa wakaanza kupigwa marufuku na waume zao kununua vitu kwa dada uyo kisa utovu wake wa nidhamu kwa mume wake.

Pia wengi hawakutaka wake zao wawe na yale mazoea ya karibu naye biashara yake ikabuma wateja wakapungua akaandamwa na kashfa ya uscan.

Eti anachukua pesa za watu ila hawatumii bidhaa zao hajatulia baba mwenye nyumba wake amemuambia anataka kuuza nyumba yake atafute sehemu ya kukaa.

Kipengele kinakuja.​
 
Sasa mbona kwenye hiyo scenario yako sijaona laana ikitumika au kuhusianishwa mkuu
 
Ndio maana nilitoa ushauri kuwa Nyuzi kama hizi hazina maana kubaki ziwe zinafutwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…