Kumbe Perfect Chikwende amevunja mkataba na Simba

Mario Kempes

Member
Joined
Jun 29, 2021
Posts
63
Reaction score
122
Kwa mujibu wa kipindi cha michezo cha clouds fm cha asubuhi hii ya leo, Perfect Chikwende ameamua kuvunja mkataba na simba na kurejea kwao Zimbabwe ambapo kwasasa anafanya mazoezi na klabu ya fc Platnum. Simba mbona mnatufivha kwenye hili?
 
Kwa mujibu wa kipindi cha michezo cha clouds fm cha asubuhi hii ya leo, perfect chikwende ameamua kuvunja mkataba na simba na kurejea kwao zimbabwe ambapo kwasasa anafanya mazoezi na klabu ya fc platnum. Simba mbona mnatufivha kwenye hili?
Ndio unajua hili leo? Wala hawajaficha ila sema ulikuwa haujapata taarifa
 
Kwa mujibu wa kipindi cha michezo cha clouds fm cha asubuhi hii ya leo, perfect chikwende ameamua kuvunja mkataba na simba na kurejea kwao zimbabwe ambapo kwasasa anafanya mazoezi na klabu ya fc platnum. Simba mbona mnatufivha kwenye hili?
Hata wasipokuambia haina effect yoyote kwako
 
Kwa mujibu wa kipindi cha michezo cha clouds fm cha asubuhi hii ya leo, perfect chikwende ameamua kuvunja mkataba na simba na kurejea kwao zimbabwe ambapo kwasasa anafanya mazoezi na klabu ya fc platnum. Simba mbona mnatufivha kwenye hili?
Isingekuwa rahisi ww kupata taarifa za simba maana huhusiki kwa lolote na kwa sasa usitemee kupata taarifa za simba kienyeji,it's very proffesional club for nowadays.
 
Chikwende Simba walikurupuka,ukiona Chikwende Simba wamekubali avunje mkataba basi jua kuna mchezaji bora zaidi ya Chikwende anatakiwa na Simba.
 
Kuna sajili kibao za Simba hela imepotea bure
 
Bado mambo ya kiswahili yanadumaza timu za tanzania

Mchezaji anasajiliwa kwa performance ya mechi moja.kisa kafunga goli.

Kwny nafasi ya chikwende palikuwa na wachezaji wengi tu wazuri ambao hawakuwa wakianza first 11.
kahata, bwalya, ajibu, ndemla,nk

Mahitaji ya timu kiufundi hayatazamwi..kuna wakt yanga iliwahi kujikuta ina right beki wanne wenye kiwango kinachofanana.
 
Kwa wanaojua mpira siku zote usajili ni kama bahati nasibu. Unaweza kumchukua mchezaji mzuri a
Waobeza sajili za Simba hawajui timu kama Tp mazembe huwa inasajili wachezaji kibao. Imagine watoto kama Singano n yule wa Mbeya city walichukuliwa na Mazembe na sidhani hata kama walipata nafasi za kucheza.

Sent from my PBAT00 using JamiiForums mobile app
 
Usajili wowote ule ni pata potea mkuu. Unaweza kumsajili mchezaji aliyekufunga au uliyemuona kwenye mechi moja na akawa mzuri kwenye timu yako.
Mfano Miquessone.
Unaweza ukafanya hivyo na mchezaji huyo asing'are, mfano Chikwende.

Unaweza kumfuatilia mchezaji kwa misimu hata mitatu na akaja kuharibu kwenye timu yako, na pia unaweza kumfuatilia mchezaji kwa muda mrefu na akang'ara kwenye timu yako.

Usajili wa Chikwende ulikua ni sehemu ya kuongeza upana wa kikosi kwa ajili ya mambo ya Covid 19. Kwahiyo hoja yako kwamba alisajiliwa wakati kuna mtu au watu kwenye nafasi anayocheza, inakosa nguvu kutokana na hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…