Kumbe Shetani Alikuwa Mwandishi wa Habari!, na Alichomfanya Eva Bustani ya Eden ni Uandishi wa Habari?- Je Media Tuombwe Msamaha Kuitwa Shetani au?

Ua
Uandikwaji wa kistaha katika biblia huandwikwa kwa namna ya kutokupoteza maana halisi ya Jambo.:- Eg Genesis 4:1.
NLT
Now Adam had sexual relations with his wife, Eve, and she became pregnant. When she gave birth to Cain, she said, “With the Lord’s help, I have produced a man!”
 
Duu umenikumbusha bible knowledge.

Biblia kwa English inaandikwa kwa uwazi angalau.Kiswahili unatumia nguvu kubwa kuelewa!
 
una mapepo
 
Nimesikitika sana Paskali anapopotosha maandiko ya biblia na kuja na tafsiri yake , hata siku moja tunda walilokatazwa siyo tendo la ndoa.

Paskali anapinga kitu lakini ukweli unaonekana hapa hapa yeye kama mwandishi akifanya ushetani wa kupotosha.
 
Pamoja na kujionesha kuwa kuwa ninyi waandishi mna uwezo wa kuelewa mambo ambayo hayakuelezwa kwa uzuri.
Ninasikitika kuwa. Si kweli.
Pia pamoja na kusema kuwa mhubiri mmoja ames3ma kuwa shetani alikuwa mwandishi wa habari, japo ambalo limefanya u defend taaluma yako kwa KUMKOSOA wewe pia kwa UKATOLIKI wako umesimika mizizi ya Uelewa wa dhambi hiyo unayoiita ya "Asili"katika upotofu mkubwa.
Yaani hauna utegemezi kwenye Neno la Mungu lililo wazi bali una hadithi au Mapokeo yako, kama ingekuwa usukumani tungekuita ngh"undya yaani Kupe kama ni mmea basi ni ile saprophytic .
1. Hoja yako imepingana na maandiko KABISA kwa kujenga wazo kuwa tendo lenyewe lilikuwa kuchi kuchi a.k.a unyumba

2. Ingekuwa swala la ki nchi ulikuwa na kosa la kuleta tafulani kwa raia na jamii ,maana kumbe jambo lenyewe ambalo watu wanagharamia ni Dhambi.
3. Kwamba tendo hilo limezuiliwa tena kwa ulinzi wa malaika akiwa na upanga wa moto.
Kwa kuwa ni m Rc na mkristu unayesali sehemu nyingi tena ukiamini Biblia kama kitabu kitakatifu ichukue usome aya hizi.

"Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Mwanzo 1:28
Wewe umeleta wazo tofauti na Muumbaji aliyewaumba na kuwaamru WAKAZAANE. Je wangezaana bila kujamiana? Ikiwa tu hata wanyama waliamriwa hivyo je wanadamu..

" Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Mwanzo 2:24

Neno Mwanaume ....na mkewe"
Ni zaidi ya jinsi bali ni status. Mtu kuwa mke wa... inambatana na tendo la ndoa ndio maana ,Neno la Mungu limeeita Ndoa ni Takatifu kwa kuwa ndio taasisi iliyoasisiwa na Mungu mwenyewe.

Na unaukataa ukweli kuwa Mungu aliuumba uuume na uke kwa matumizi sahihi na umempatia credit shetani kuwa aligundua matumizi ya kile alikiumba Mungu.

Kwanini nasema umeleta TAHARUKI. Umeatishia kuwa kwa mjibu wa tafasri yako mti wenye tunda unalindwa.

" Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima.
Mwanzo 3:24

Lakini kwa hili nasimama UPANDE WAKO. Huyu mhubiri anasema shetani alikuwa mwandishi wa habari anapotosha watu na kuleta watu kuifikiria vibaya taaluma nzuri ambayo mimi najua haina ubaya.
Namjua Musa kama mwandishi wa habari wa mwanzo mwanzo. Kwa sababu
1. Aliweza kupeleka taarifa juu ya Mungu kwa jamii ya Kiebrania wakiwa Misri. Jambo ambalo taaluma hii HUFANYA ikipeleka taarifa au maarifa sahihi kwa jamii. Si maarifa bali ni wapasha habari ili jamii ijue nini kinaendelea
2. Musa aliandika taarifa hizi katika maandishi, ili zisomwe na wengi lakini akiweka kumbukumbu.

"Tena Mungu akamwambia Musa, Waambie wana wa Israeli maneno haya, Bwana, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.
Kutoka 3:15
Musa ni mpeleka habari

Kwa fungi hili Mungu ndio Mwalimu wa Kwanza wa uanahabari.

Kama watu wa namna hii wakiachwa pasipo kuambiwa watapotosha wengi na kujenga CHUKI ya taaluma hii
Taaluma hii ni nzuri ikitumiwa kwa UZURI.

HITIMISHO
1. Tofasri ya kula tunda ulioweka inapingana na Biblia yote , lkn hata inapingana na logic za kawaida za kuwazua mambo. Ina ukinzani mkubwa.
2. Uandishi habari ni mzurina huenda kila mtu ni mwandishi wa habari japo anaweza asiwe rasmi au kusoma chuo. Shetani yeye ni muovu na ni mwanzilishi wa huo.

I salute ur post.









Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Umesema dhambi ya asili ni mchakato wa kupata kiumbe kingine; biblia inasema baada ya kuwapulizia pumzi ya uhai akawabariki na kusema "zaeni mkaongezeke". Hebu tuambie process za kuzaa kabla na baada ya hiyo dhambi
 
Kwa hio hapa ndugu muandishi unamaanisha kwamba shetani alilala na Eva wakala tunda mujarabu na baada ya kumaliza Eva kuona utamu wa tunda akatoka akaenda kwa Adamu akamuomba ampe na yeye tunda ale yaan alale nae baada ya kulala na shetani, in short shetani ndie alieanza kulala na Eva sio Adamu

Asante sana kwa kunifungua akili..

Wewe ni muandishi na mfafanuzi mzuri sana wa biblia yaan haufifichi mambo unaweka waaazi kabisa
 
Mungu akauliza: Adamu uko wapi?

Adamu: Nipo uchi?

Mungu akauliza: umekula lile 'tunda' nililowakataza msile?

Adamu: Huyu mwanamke uliyeniletea ndie 'alienishawishi'...
 
Mwaka 2010 Kuna maandishi wa habar alihenda hosptali fulani kusaka news huyo bwana alitonywa yakuwa Kuna Dr wa mchongo hosptali fulani jamaa akaweka appointment akaenda muona Dr alipo fika akahoji utaaluma wa Dr mpaka atibu wagonjwa Dr badala ya kudhibitisha taaluma yake alitoa rushwa milioni kumi tangu siku hiyo habari haikutoka.

Mfano mwingine mwandishi wa habari kuambatana na Waziri kwenda kusambaza mitungi ya Gesi kwa wananchi wasio na uwezo wa kulipa gesi uo sio ushetani?
 

Mna unyoka mwingi sana aiseee
 
Waandishi wa kitanzania ni mashetani kweli kwani wanafumbia macho maovu yanayofanywa na watawala na kugeuka kuwa "mpiga zumari wa amerini", kwa wale wahenga wenzangu watamkumbuka. Mkilambishwa asali inakuwa shida sana
 
Bonny kawakosea sawa mpigisheni magoti ila unatulisha matango pori kutuaminisha kwamba kujaamiana ndio tunda la mti wa kati.
Kilichoandikwa ni tunda kama tunda hizo tafsri za pembemi ni zenu nyie wapotovu!!!!
Adam na Hawa\Eva walishapewa kibali cha kuzaa na kuijaza dunia why tendo la uzazi unaliita dhambi ya asili?
Hivi inaingia akilini kweli tendo la kujamiiana lifichwe fichwe kwenye biblia wakati zama za luth limetajwa wazi wazi na hata zama za Daud hivyo hivyo
 
Anatulisha matango pori huyu yeye alitakiwa kumpigisha goti Bony kwa kuwanasibisha na Shetani ila maandiko angeyaacha kama yalivyo kuliko alivyoandika eti Shetani kamnyandua Eva na kusepa so baada ya Eva kuwa so horny akalazimisha anyanduliwe na Adam!!!
Labda Mayalla atutatanulie lile agizo la kuijaza dunia lingetekelezekaje kama kunyanduana kulikatazwa?
Mwandishi wa habari unapotosha umma namna hii

Kama jambo ulifahamu ni bora kukaa kimya.

Mambo ya imani sio kwa kila mtu kubali yamekupita kushoto
 
Umeshapotezwa tayari
 
#Kutoka hapa mkoani Mbeya Mimi ni Isakwisa Mwaifuge wa Itv.... Ripoti imefika
Kibao kimekugeukia brother P
Usimseme mtu vibaya kwa manipulate akili za watu kupitia Maandiko.
Kitabu Cha ayubu kinaonesha shetan alikuwa akipeleka ripoti na malalamiko kwa Mungu kumhusu Job..... Mhandishi si m2 wa kuripoti matukio km alivyofanya shetani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…