The Khoisan
JF-Expert Member
- Jun 5, 2007
- 16,434
- 14,547
TANZANIA ina idadi kubwa ya miti ya aina nyingi inayoweza kutumika kama tiba ya maradhi mbalimbali.Inakadiriwa kuna aina 15,000 za miti inayotumika kama dawa nchini, lakini Watanzania hawafaidiki na mauzo ya dawa zenyewe, yanayokadiriwa kuingiza Dola za Marekani bilioni 1.6 kwa mwaka.
Cha kusikitisha ni kwamba, kimataifa asili ya dawa hizo haisemwi kuwa ni Tanzania.
Umuhimu wa dawa za zinazotokana na miti, unajionyesha hasa kwa kuwa asilimia 60 ya Watanzania hutegemea tiba asili kwa matibabu yao.
Tukio la mwaka 2011 la Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapila wa Loliondo mkoani Arusha, kuuza dawa yake maarufu kama kikombe cha babu , liliibua hisia nzito baada ya watu wa ndani na nje ya nchi kufurika katika kijiji cha Samunge ili kunywa dawa hiyo.
Hata hivyo, dawa hiyo iliyopimwa na wataalamu na kuthibitishwa kutokuwa na sumu, huku bado ikiendelea kufanyiwa uchunguzi, ilishuka umaarufu wake ndani ya kipindi kifupi. Dawa hiyo sasa imebaki historia.
Kwa kutambua umuhimu wa dawa za asili kijamii na kiuchumi, watafiti na waganga wa tiba za jadi walikutana jijini Dar es Salaam hivi karibuni kujadili umuhimu huo na kuweka mikakati ya kiutafiti ili kukuza biashara na matumizi yake.
Mkutano huo pia uliwahusisha wataalamu kutoka vyuo vikuu vya Dar es Salaam, Malawi, Namibia, Wits, Pretoria CSIR, TRFCA na ACGT.
Soko la dawa za asili
Akifafanua kuhusu soko na fursa ya kuuza dawa za asili kimataifa, Mkurugenzi wa utafiti wa tiba asili katika Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dk Hamisi Malebo, anakariri takwimu za Shirika la Afya duniani (WHO) linalosema kuwa, asilimia 80 ya watu duniani hutegemea tiba asili.
Anaongeza kuwa kati ya asilimia 25 hadi 40 ya dawa zote, hutokana na mimea huku asilimia 40 hadi 50 hutokana moja kwa moja na dawa za asili au kuiga viini vya mimea.
Kwa jumla kuna zaidi ya jamii 50,000 za mimea duniani hutumika kama dawa, anasema na kuitaja India kuwa ndiyo nchi yenye aina nyingi za miti ya dawa duniani ambayo ina kati ya jamii 15,000 hadi 20,000.
Nchi nyingine anayoitaja ni China inayoongoza kwa kuuza dawa hizo duniani ikiwa na jamii zipatazo 5,800 tu.
Mahitaji ya dawa katika nchi zilizoendelea kwa viwanda, ambako watu wanakimbilia kwenye miti dawa, yanaongezeka siku hadi siku. Kwa mujibu wa WHO, dawa za asili zitafikisha mauzo ya Dola za Marekani trilioni tano ifikapo mwaka 2050, ambapo kwa sasa yanafikia Dola 80 bilioni kwa mwaka, anasema na kuongeza:
Hii inaonyesha mwelekeo mzuri na mahitaji ya dawa hizo, hivyo inahitaji kukumbatiwa kwa kuboresha uanzishaji, uzalishaji na mikakati ya biashara kwa Tanzania ili kukuza mauzo ya nje.
Soko la kimataifa
Akieleza jinsi soko la kimataifa linavyohitaji dawa hizo, anasema India na China ndiyo zinazoshikilia usukani ambapo kwa mwaka 2007, kulikuwa na mauzo ya Dola za Marekani bilioni 75, huku China pekee ikiuza asilimia 24 na kufuatiwa na India na Thailand.
Anasema, China huuza tani 120,000 za dawa za asili nje wakati India inafuatia kwa kuuza tani 32,000. Kwa pamoja nchi hizo ndio vinara wa soko la kimataifa.
Anaitaja pia India kwa kuongoza kuuza zao la Mlonge kwa kiasi cha tani milioni 1.3 kwa mwaka na hivyo kuingiza Dola za Marekani 6 bilioni.
Bara la Ulaya huingiza tani 400,000 za dawa za asili kwa mwaka, zikiwa na thamani ya Dola za Marekani Dola bilioni moja kutoka Afrika na Asia.
Source: Mwananchi