Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
MKATABA WA KUMWEKA FELIX TCHISEKEDI MADARAKANI
Mnamo Tarehe 22/11/2018, siku ya Alhamisi katika eneo la Upper Hill kwenye ofisi ya Mzee RAILA AMORO ODINGA kulifanyika mkutano, Ajenda kuu ya mkutano huo ilikuwa ni jinsi ya kuchukua madaraka ya Congo baada ya JOSEPH kumaliza muda wake;na pia kupanga mikakati mahsusi ya uendeshaji wa Kampeni za mgombea wao.
Mkutano huo ulihusisha wajumbe kutoka Rwanda, Uganda, Congo na Kenya. Aidha, Wajumbe wote waliohudhuria walibeba masharti yenye maslahi kwa nchi zao.Mathalan, Uganda ilikuja na masharti kuwa kama FELIX TCHISEKEDI angelitaka kuungwa mkono na Uganda katika kampeni za Urais; yafuatayo yalipaswa kuzingatiwa:
Kampuni ya mafuta ya TOTAL inabakia nchini DRC hata baada ya kushika Madaraka ya nchi hiyo. atakaposhika madaraka.
Akubali kuacha huru kikundi cha waasi wa ADF kuendelea kufanya harakati zake nchini Congo.
Kwa upande wa Rwanda,ilikuja na masharti yafuatayo:
FELIX TCHISEKEDI amsaidie kumng’oa Mamlakani PETER NKURUNZINZA, Rais wa Burundi
Awaache huru Wanyamurenge walioko DRC na akubali kuwapatia Wilaya.
Amuachie Jenerali PAUL KAGAME jimbo la Kivu ya kusini kama kitega uchumi chake
Ni Dhahiri kuwa masharti hayo yaliwekwa na kwa shinikizo la Marais YOWERI KAGUTA MUSEVENI wa Uganda na PAUL KAGAME wa Rwanda. RAILA ODINGA kwa upande wake kama muwakilishi wa Kenya hakuweka wazi masharti ya Kenya.
Mwanzo FELIX TCHISEKEDI hakukubaliana na masharti hayo na kusema kuwa yeye hayupo tayari kukubali masharti hayo maana lengo lake ni kutafuta suluhu ya Kivu ya kaskazini na Kivu ya Kusini. Baada ya Tchisekedi kusita, walikaa kando RAILA ODINGA, FELIX TCHISEKEDI na VITALI KAMERHE na baada ya kurejea ukumbini FELIX alikubali kusaini nyaraka za makubaliano. Hapo Rwanda na Uganda wakapitisha kuwa mgombea na kuahidi kumuunga mkono na kumsaidia katika gharama za kampeni.
MUTOMBO LAURENT ndiye aliyekuwa muwakilishi kutoka Kinshasa alitumwa na Rais JOSEPH KABILA kuja kushuhudia makubaliano hayo. Sharti la Rais JOSEPH KABILA lilikuwa kwamba FELIX TCHISEKEDI akikubali kusaini mkataba wenye masharti ya Uganda na Rwanda basi JOSEPH KABILA ataridhia kumuachia madaraka na kuhakikisha kuwa FELIX TCHISEKEDI anakuwa Rais mpya wa Congo kwa gharama yoyte ile.
Kesho yake, ilikuwa tarehe 23/11/2018 ilikuwa ni siku ya kuhitimisha mikataba ilisainiwa. Mkataba huu ulikuwa ni muendelezo wa mkataba ambao ulimwingiza JOSEPH KABILA madarakani kufuatia kifo cha Rais LAURENT DESIRE KABILA. Kwa mantiki hiyo, kuna uwezekano mkubwa kuwa generali PAUL KAGAME na YOWERI KAGUTA MUSEVENI kuhusika na kifo cha Rais LAURENT DESIRE Kabila. Hii ilifanyika ili kupata mwanya wa kupora mali ya Congo kwa urahisi. Sasa mkataba huo umegeuzwa kuwa moja ya vigezo vya kuwa rais wa Congo.
Mapema tarehe 27/11/2018 sherehe ya kifahari ilifanyika Jijini Nairobi Kenya kwa lengo la kuweka wakfu muungano wa chama cha UDPS cha FELIX TCHISEKEDI na chama cha UNC kinachoongozwa na VITAL KAMERHE. Muungano kati ya vyama hivi viwili unafahamika kama CACH.