Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Nilikutana na mzee mmoja mwenyeji wa mkoa wa Mara akanieleza hii kitu,ndipo nikaamua kujaribu kuuliza na kukutana na kijana ambae alithibitishia kuwa jambo hilo lipo.
Jambo lenyewe ni kuwa, kuna dawa ya mitishamba ambayo ukichanjwa kisha ukapakwa hautakufa mapema. Hii maana yake ni kwamba ukishapakwa dawa hiyo,unakuwa na "machale" kabla ya kuikaribia ajali au jambo lolote la hatari,pia hautaugua maradhi au kama ukiugua haufi,hii ina maana kuwa kuna uwezekano mkubwa wa wewe kufikia uzee.Huko uzeeni utazeeka mpaka utakua ni wa kubeba.
Ikitokea ukapata maradhi uzeeni bado hutakufa, bali unaweza kuanza kuoza baadhi ya sehemu za mwili jambo litakalopelekea funza kutoka na chuma ulimo kuanza kutoa harufu kali.
Mtu aliefikia hatua hiyo kama ndugu wakihitaji afe basi hutakiwa kutoa bati au nyasi ili mwanga wa jua uingie ndani na kitendo hicho humfanya kikongwe huyo kufariki.
Jambo hili limeniacha mdomo wazi hasa nilipokutana na huyu kijana aliyethibitisha hili.
Je hapa JF kuna aliyewahi kusikia au kushuhudia hii kitu?Au kuna mwenye ujuzi wa hii kitu atujuze?