Kumbe urais wa Marekani ni kama ufalme?

Kumbe urais wa Marekani ni kama ufalme?

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Jana, rais mteule Donald Chizz Trump, aliwateua vivyele vyake yaani mkwe wa mwanae wa mwisho Tiffany mwarabu aitwaye Boulos kuwa mshauri wake wa masuala ya mashariki ya kati na mkwe mwingine wa binti yake Bianca, aitwaye Charles Kushner kuwa balozi wa Marekani nchini Ufaransa.

Hapa Trump atatuponza nchi za kiswazi. Sitashangaa kusikia Abduli au Wanu wameteuliwa washauri wa maza hata mawaziri. Kweli demokrasia sasa ni domogasia kama siyo demockery. Kwa sasa akina M7 na maimla wenzake wanashangilia.

Theodoro Obiang Nguema wa Equatorial Guinea alilijua hili zamani hadi akamteua mwanae Theodorin Obiang Mangue kuwa makamu wa rais wakati mdogo wake mwingine Gabriel Obiang Mbega Lima waziri wa fedha na mipango. Akina Ridhiwan Kikwete sasa hawana wasiwasi na ulaji wao. Ama kweli wamejua kututenda.
 
Kwa makusudi mazima umeamua kutumia neno "ufalme" kwa nia ovu kwa muktadha uliopindishwa.

Ufalme ni aina ya utawala wa nchi ambao mtawala hupatikana kwa kurithi mara nyingi kutoka kwa mzazi wake. Inapotokea mtawala hana mtoto (imetokea Oman utawala uliopita) au anayepaswa kurithi hataki urithi (imetokea Uingereza kwa Albert kaka yake Mfalme George, baba yake Queen Elizabeth II) basi ufalme humwangukia ndugu wa karibu au wosia wa mfalme kama ilivyotokea kwa nchi hizo mbili.

Donald Trump hakuchukua utawala kwa mojawapo ya njia hizo mbili. Aidha, Katiba ya Marekani haimruhusu kurithisha nafasi yake.
 
Back
Top Bottom