Elections 2010 Kumbe walilipwa kuhudhuria mkutano wa CCM Dar!

Elections 2010 Kumbe walilipwa kuhudhuria mkutano wa CCM Dar!

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
239

Wananchi wengi katika umati mkubwa wa watu waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM kule Jangwani siku ya Jumamosi iliyopita walifika hapo baada ya kuliupwa kufanya hivyo.

Baadhi ya watu niliozungumza nao wanaotoka sehemu za Mbagala Rangi Tatu na Mbande wanasema mabasi ya daladala yalikodishwa na CCM kusomba watu kuwaleta jijini kuhudhuria mkutano na waliokubali kupanda walilipwa Sh 5,000 kwamba hizo fedha ni za usumbufu na nauli yao ya kurudi baada ya mkutano.

Kila moja ya mabasi haya yaliyokodishwa yalikuwa yanalipwa mapato yao ya siku mbili.

WanaJF, hizi habari ni za uhakika nilizopata kutoka kwa watu watatu waliopanda mabasi hayo na kulipwa kutoka sehemu hizo mbili nilizotaja. Wanasema tangu asubuhi majira ya saa 3 mabasi yalifika maeneo hayo na kuegesha huku viongozi na makada wa CCM wakihamasisha watu kuingia. Sh 5,000 ni nyingi sana katika sehemu hizo.

Hali hii bila shaka ilijitokeza katika sehemu nyingi tu pembezoni mwa Jiji siku hiyo – watu kulipwa na kutafutiwa usafiri ili wahudhurie mkutano.

Mapesa yaliyotumika ni mengi kwa tafsiri yoyote ile, na bila shaka ni kati ya zile Sh Bilioni 50 ambazo CCM imetenga kwa ajili ya kampeni mwaka huu.

Tatizo langu hapa si uhalali au la kwa CCM kulipa watu kuhudhuria mkutano wao wa kampeni, ingawa pengine ni suala linaloweza kutazamwa kama ni njia mojawapo ya kuwahonga wapiga kura.

Tatizo langu hasa ni ile dhana inayojengwa kwamba CCM bado ina wafuasi wengi, dhana ambayo siyo kweli kwani iwapo wananchi wangeachwa kufika hiari yao, mkutano ule ungehudhuriwa labda na nusu tu ya watu waliojitokeza.

Wanachofanya CCM ni kujenga muonekano wa ufuasi mkubwa katika mikutano yao kwa nguvu fedha walizonazo – na siyo kwa hiari ya wananchi wenyewe bila kushawishia kwa njia ya pesa.
 
kaka hiyo ni tactic ya vita.

lazima umtishe adui wako.

kama pesa zilizotumika ni halali basi hapa inabidi tuipe point ccm kwa kuweza kuwa na mbinu za kuwatisha wapinzani wake. iko katika njia za kujihakikishia inapata ushindi tu.

lakini hizo pesa kweli za halali?
 
Mimi naweza kuamini kwani nilipita maeneo ya Magomeni, Mabibo na Kawe nikaona daladala zaidi ya moja zikiwa zimeegeshwa kwenye ofisi za CCM zikiwa na mabango ya CCM huku watu wakihamasishana kuwahi kwenye mkutano wa ufunguzi. Sikuweza kujua mara moja kama magari hayo yalikodiwa na wanachama wenyewe au waliwezeshwa.
 
BASI KAMA HALI NI HII INATISHA SANA!..I wish ningalikuwa ndo mgawaji wa hizo pesa..huh!
 
Very sad, najua hata ingewafikia TAKAKURU wasingefanya lolote

TAKAKURU wanasubiri VYAMA vya Upinzani vianze kampeni hili viwakamate
 
Ni mbinu tu hizo na kawaida yao kutumia pesa kufanya chochote halali na haramu!
 
Wanachofanya CCM ni kujenga muonekano wa ufuasi mkubwa katika mikutano yao kwa nguvu fedha walizonazo – na siyo kwa hiari ya wananchi wenyewe bila kushawishia kwa njia ya pesa.

Wwnafanya hivyo ili iwe rahisi kuchakachua KURA
 
I wish mwaka huu kutatokea ***************************** nyie subirini tu mtaona matokeo yake.
 
Pathetic..... !!!!

Leo Clouds wamekuja na mpya, katika kipindi cha pawa brekifast cha magazeti walikuwa wanasoma habari zilizoko kwenye gazeti la Mtanzania juu ya maisha binafsi ya Dr. Slaa, kwa mtazamo wangu wa harakaharaka lazima kuna pesa imetembea kwa magazeti hayo kusomwa redioni. kwani wanajua kabisa bila kufanya hivyo ni watu wachache sana ndo wangelipata habari zake kutokana na ukweli kwamba magazeti ya New Habari Cooperation hayasomwi na watanzania wengi. Kwa hiyo kwa habari yoyote iliyoandikwa humo kuwafikia watanzania lazima yasomwe redion na nina imani akina PJ na wenzake wamekula hela nzuri kwa kulisoma Mtanzania leo
 
Basi itakuwa ni bahati mbaya sana, maana waliambulia kuona anavyoanguka badala yahotuba
 
Hiyo ni kweli kabisa maana juzi nilikuwa moshi na nilishuhudia live na mi pia nikalamba buku tano na nilivyofika kwenye mkutano wao tu nikatorokea kwenye bia.
 
Pathetic..... !!!!

Leo Clouds wamekuja na mpya, katika kipindi cha pawa brekifast cha magazeti walikuwa wanasoma habari zilizoko kwenye gazeti la Mtanzania juu ya maisha binafsi ya Dr. Slaa, kwa mtazamo wangu wa harakaharaka lazima kuna pesa imetembea kwa magazeti hayo kusomwa redioni. kwani wanajua kabisa bila kufanya hivyo ni watu wachache sana ndo wangelipata habari zake kutokana na ukweli kwamba magazeti ya New Habari Cooperation hayasomwi na watanzania wengi. Kwa hiyo kwa habari yoyote iliyoandikwa humo kuwafikia watanzania lazima yasomwe redion na nina imani akina PJ na wenzake wamekula hela nzuri kwa kulisoma Mtanzania leo
Ndio ofutopic hizi tunazisemaga.Title ya habari haihusiani kabisa na haya maelezo waliyotoa,Halafu huna hata ushahidi wowote kwenye habari yako.Poor you!
 
Ndio ofutopic hizi tunazisemaga.Title ya habari haihusiani kabisa na haya maelezo waliyotoa,Halafu huna hata ushahidi wowote kwenye habari yako.Poor you!

My Daughter, habari inahusu thithiem kutoa pesa kwa watu kuhudhuria mkutano, hapa najadiri uwezekano wa pesa kutembea katika kusambaza habari za kumpunguzia umaarufu mgombea fulani.... tofauti yake ni nini kati ya hizi habari. Nadhani wewe ndo unashida ya kuelewa... usibebe kama mawe, tafakari!!!!!!!!!!
 
Pathetic..... !!!!

Leo Clouds wamekuja na mpya, katika kipindi cha pawa brekifast cha magazeti walikuwa wanasoma habari zilizoko kwenye gazeti la Mtanzania juu ya maisha binafsi ya Dr. Slaa, kwa mtazamo wangu wa harakaharaka lazima kuna pesa imetembea kwa magazeti hayo kusomwa redioni. kwani wanajua kabisa bila kufanya hivyo ni watu wachache sana ndo wangelipata habari zake kutokana na ukweli kwamba magazeti ya New Habari Cooperation hayasomwi na watanzania wengi. Kwa hiyo kwa habari yoyote iliyoandikwa humo kuwafikia watanzania lazima yasomwe redion na nina imani akina PJ na wenzake wamekula hela nzuri kwa kulisoma Mtanzania leo

Mkuu ungeanzisha thread nyingine.
 
Hii ni habari nzuri kwani it is somewhere in history kwamba tawala nyingi za kidhalimu huenda mpaka kwenye level ya kukosa umaarufu na hata kuaminiwa na wananchi wake as such hulazimika kuweka kila kitu at a price. Mwisho wa siku dhamira hushinda bei.

Sasa bssi CCM kwa jinsi ilivyokuwa out of touch inapata shida mno kutokana na kupendwa Dr. Slaa ambayo ni free of charge affection. CCM ingeweza kumcrash Slaa ina day kama mchuano ungekua ni nani ana hela zaidi lakini the game is just different and too different.

Wewe subiri uzinduzi wa kampeni ya Slaa, utawasikia tu CCM malalamiko ya kienyeji...............
 
Nadhani CCM wamegundua hawana mvuto mbele ya jamii ndiyo maana wameamua kutoa fedha kwa wananchi ili mikutano yao ionekane ina watu.Mama Batilda Buriani alipokuwa akirejesha fomu watu waliomsindikiza walilipwa fedha sielewi mikutano yake atakuwa akigawa fedha au vipi ?.
 
Shule za kata ndiyo kiama cha ccm. Hizi shule ijapokuwa siyo za kiwango sana bado form four leaver au failure siyo std seven leaver lazima kuna kitu atakipata. Hiki ndiyo kizazi kitakachoibomoa ccm na kuipa chama mbadala nafasi. Chadema ina nafasi nzuri sana hasa kwa wale ambao wameweza kusoma sera zake na siyo kusikia majina ya viongozi tu na kuanza kuyajadili.
Ccm inapofikia umma unanunuliwa kuja kwenye mikutano basi ni hatari. Hata hivyo inakuwa ni mbinu mbadala kwa helikopta. Ifikie wakati vyama mbadala viweze kuwashawishi vijana katika level ya chini wajiandikishe kupiga kura na wajue nini cha kuangalia ktk chama na mgombea wake.
Imani potofu itapotea na watu wote watakuwa wanajua nini cha kufanya wakati wa uchaguzi.
 
wezee wetu walisema,

"KIZURI CHAJIUZA, KIBAYA CHAJITEMBEZA"

We all know kipi ni KIZURI, kipi ni KIBAYA,

Huu ndio wakati mwafaka wa kununua "KIZURI"
 
Back
Top Bottom