Elections 2010 Kumbe walilipwa kuhudhuria mkutano wa CCM Dar!

:confused2:hawa sisiemu!!:confused2::confused2:aaaah! sijui kwa kweli......enewei Mungu jalia Slaa awe raisi
 
Wataendelea kusomba watu hadi lini, kitendo hicho kinapunguza imani ya wanachama kwa chama husika kuwa siku wakikosa hizo pesa ndio utakuwa mwisho wa chama.
 
Wataendelea kusomba watu hadi lini, kitendo hicho kinapunguza imani ya wanachama kwa chama husika kuwa siku wakikosa hizo pesa ndio utakuwa mwisho wa chama.

Hawawezi kukosa hela, wataiba tu. Sasa hivi wanatumia za Kilimo kwanza na miradi minginine ya kisanii kama vitambulisho vya kitaifa na mradi wa barabara za juu kwa juu.
Mwakani watabinafsisha JKT kwa waarabu , na hapo watalamba peasa zingine za 2005.
Hawa watu wamchanganyikiwa, hivyo wako tayari hata kuua ili wajihakikishie madaraka walindane. Ndiyo hulka ya viongozi wezi na wadhalimu.
Bila kuwa ngangari na kupigania haki zetu, mchezo huu utaendelea sana.......ni lazima tupiganie uhuru mpya....
CHADEMA mwaka huu wangeshinda, kama tu kungekuwa na tume huru ya uchaguzi. Kinachonishangaza ni vyama vyenyewe kuingia kwenye uchaguzi ambao tayri matokeo yake yamepangwa na NEC.
 
ndugu huo ndio ukweli wenyewe, japo kuna watu wanakataa kabisa kuwa hawakulipwa lakini mimi nina rafiki zangu wawili wamesema kweli wamelipwa buku 5 kuhudhuria pale.
hii ni njia ya CCM katika mkakati wao wa kuiba kura, lakini hawa watu bado mimi nawaona kuwa hawana akili kwa sababu wanadhani mtu akihudhuria mkutano wao wa kampeni ni lazima aipe kura CCM. Raia yeyote na mwanachama wa chama chochote anatakiwa kuhudhuria mikutano ya kampeni ya vyma vyote ili apate kujua sera na yale yatakayofanywa pindi watakapopewa ridhaa ya kuongoza.sasa utasemaje kuwa wote wanaohudhuria mkutano wa kampeni wa CCM ni wapenzi wa CCM au wote wanaohudhuria mkutano wa kampeni wa CHADEMA wataipa kura CHADEMA
 
Kama hizi habari ni za kweli na kama ushahidi upo, kwani wapinzani hawawezi kwenda mahakamani kuzuia uchaguzi usifanyike? :confused2:
 
teh teh teh, ni kweli kabisa kwamba ccm imepoteza mvuto, na hakuna anesikia fahari kuwa mwana ccm, na ndio maana wananunua watu kwenda kwenye campain, lakini toka moyoni hao watu hawaipendi ccm na hakika hawataipigia kura.
ukitaka kujua kua ccm imepoteza mvuto, we angalia huko mtaani kama utakuna na watu wangapi waliovaa fulana na kufika za chagua kikwete, chagua ccm kama ilivokua mwaka 2005, kila kuta za nyumba, gari, mpaka mikokteni ilikua na chagua ccm, sasa hivi vinaonekana?
wanaweza kuwanunua watu waende kwenye mikutano, lakini hawawezi kuwalazimisha kuvaa fulana na kufia zao.

mwaka 2010 "ccm wameangukia pua"
 
wote wanaohudhuria mkutano wa kampeni wa CCM ni wapenzi wa CCM au wote wanaohudhuria mkutano wa kampeni wa CHADEMA wataipa kura CHADEMA

Kwa tume ipi? hii iliyoteuliwa na mgombea urais au yakwako wewe?
 
twanaweza kuwanunua watu waende kwenye mikutano, lakini hawawezi kuwalazimisha kuvaa fulana na kufia zao.

mwaka 2010 "ccm wameangukia pua"

Lakini ikifika october 31 CCM watachukua wataweka waaaaa au SIO????
 
Very sad, najua hata ingewafikia TAKAKURU wasingefanya lolote

TAKAKURU wanasubiri VYAMA vya Upinzani vianze kampeni hili viwakamate

Mkuu ni nani kukuambia TAKUKURU ipo kwa maslahi ya wote? Hiki ni chombo cha serikali iliyoko madarakani ambayo inaongozwa na chama tawala kwa sasa!! Yale maadnishi ya kuundwa kwa vyombo hivi na nguvu zao kisheria ni viini machot tu, practically havitekelezwi!! Ukiona vinatekelezwa basi ujue kuna filimbi imefyetuliwa na mkuu!! Yaani Hoseah aende kinyume na bosi wake aliyemteua? Hii haingii akilini kabisa. Wewe subiri kina CUF na Chadema waaanze shughuli uone vijana wa Mwema na Hosea watakavyokuwa mbogo!! Wawili hawa you connect the dot!!
 

mpwa niwezeshe nitazisomea wapi hizo sera maana chadema naikubali kwa sana.!
 

Hawa Clouds wako kibiashara zaidi na mwaka huu washaona kutakuwa na fungu la uchaguzi na ndo maana mapema wakaanza kujipendekeza ili watafune hili fungu. Sasa chama kipi kina fungu kubwa la mihela kama sio CCM?!
 
Vyombo vya dola pia vililipwa sasa nani atakamata nani
 

Kama ni kweli basi nakisikitia sana Chama changu.Its bending too low!!
Kutoka mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la Arusha, azimio la makabwela, watu waliandamana wakiwa wamebeba matawi mazima mazima tena kwa kilometa zaidi ya 10 kutoka Temeke,Ilala Magomeni kumshangilia Mwalimu.
Leo watu waenda kwa mshiko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…