Kumbe, Twilumba, mimi napenda lugha ya Kiswahili sana tena sana! Binafsi nafikiri kwamba ni lugha bora! Ni nani anayeweza kudharau lugha ya Kiswahili? Hamna mmoja! Au kusema ni lugha duni? Hamna hata mmoja! Hayupo – isipokuwa anakosa sana. Miaka kadhaa iliyopita nilinunua vitabu vya shule ‘Tujifunze Lugha Yetu'. Vilinisaidia saaana kujifunza Kiswahili. Nilisoma kama mtoto. Nilijifunza kama mtoto – nilifurahia sana kufanya hivyo. Sasa je, naweza kukuvuta ukubali nami ya kwamba ……..inawezekana…….. labda …… yupo mzungu mmoja duniani anayependa lugha ya Kiswahili toka moyoni mwake bila kutafuta faida yake yenyewe??? Unafikirije?